Wednesday, September 24, 2014

DUNIA SIJUI INAKWENDA WAPI??: MWANAMKE HUYU ATUMIA ZAIDI YA MILIONI 30 KUONGEZA TITI (ZIWA) LA TATU MWILINI MWAKE ILI APATE USTAA KWENYE TV

Jasmine Tridevil katika pozi.
Mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Jasmine Tridevil (siyo jina lake halisi) mwenye umri wa miaka 21 amedai kufanyiwa upasuaji na kuongezwa titi la tatu kupitia mahojiano aliyoyafanya redioni.
Jasmine Tridevil.
Jasmine ambaye ni raia wa Tampa jijini Florida nchini Marekani anayejishughulisha na utoaji huduma ya massage, alilipa kiasi cha dola za Kimarekani 20,000 sawa na milioni 33.4 za Tanzania kufanyiwa upasuaji huo.
Mwanamama huyo katika mahojiano na Real Radio 104.1 alidai kuwa ameamua kufanya hivyo ili asiwe na mvuto kwa wanaume na pia apate ustaa katika tv.
Lakin pia mrembo huyu wazazi wake wamekataa lakin yeye amesema lazima azma yake ya kuwa staa itimie
tayari ameshasambaza picha zake akiwa na matiti matatu ambapo yeye amesema ni furaha kwake.
Jasmine Tridevil.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI