![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi6JotY3ThscIxcX8UKNuOuYpKIOJ-tmAHbAoSTI2XeHohKxoErnu87CRS-oEL-L6llNspaCpX-pHv8lpm42RK1dEZjBcP3sSys-j5beCnY2yDmZQ6VBxjAwT-vLR_G0XOF7oNpbbO79jQ/s400/Diamond1.png)
Na Baraka Mpenja
MSANII
maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platinumz’ atatoa burudani ya kufa mtu katika tamasha la ‘Simba Day’
linalotarajia kufanyika kesho (Agosti 9, mwaka huu) katika uwanja
wa Taifa, uliopo Chang`ombe jijini Dar es salaam
Makamu
wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amezunguma na waandishi wa
habari katika ukumbi wa JB Belmont katikati ya jiji na kueleza kuwa
saabu ya kumchagua Diamond ni kutokana na ukweli kuwa ndiye msanii
anayetamba kwa sasa.
Daimond
ambaye kwa sasa ‘anasumbua’ na wimbo wa My Number One na Mdogo mdogo
ataungana na bendi ya Twanga Pepeta na wasanii wengine kama vile Dully
Sykes, Barnaba, Mataalum na makundi ya kudansi kutumbuiza katika
tamasha hilo la kila mwaka.
Mbali
na burudani hizo, kutakuwa na mechi mbili za mpira wa miguuu ambapo
timu ya vijana ya Simba chini ya miaka 20 itachuana na timu ya vijana ya
Azam fc.
Baadaye kikosi kamili cha Simba kitaoneshana kazi na Zesco United ya Zambia.
Katika
mechi hiyo, Simba imeahidi kutumia kikosi chake kamili ambapo wachezaji
wote waliowasajili majira haya ya kiangazi mwaka huu wataonekana katika
mechi hiyo maalum ya kuwatambulisha kwa mashabiki wao.
“Wachezaji wote wataonekana siku hiyo na mshambuliaji wetu mpya kutoka kenye Kiongera tayari amewasili nchini”. Alisema Kaburu.
Naye
meneja wa Zesco, Mavuto alitamba kuwafunga Simba katika mechi ya kesho
ingawa hana uhakika watawafunga magoli mangapi, lakini alisisitiza kuwa
watafanya vizuri, hivyo kuwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kesho.
0 comments:
Post a Comment