Friday, July 18, 2014

TIMU YA TANZANIA YAWASILI GLASGOW TAYARI KWA MICHEZO YA JUMUIYA YA MADOLA


Bw. Msanjila akimkabidhi bendera ya Tanzania Nahodha wa Timu hiyo Selemani Kidunda. Wengine pichani ni Kiongozi wa Msafara Bw. Mwarami Mchume na Mkurugenzi wa Michezo Bw. Leonard Thadeo.
TIMU ya Tanzania kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola imewasili katika  uwanja wa ndege wa Kimataifa Glasgow, Scotland usiku (Alhamis, 17 Julai 2014) kwa ndege ya Shirika la ndege la Falme za Kiarabu (Emirates).
Jumla ya wanamichezo 42 waliwasili Uwanjani hapo na kupokelewa  na Afisa Ubalozi wa Tanzania London Bw. Amos Msanjila. 
Pamoja na mapokezi na shamrashamra za wenyeji, baadhi ya Watanzania waishio Glasgow walikuwepo Uwanjani hapo wakipeperusha bendera za Tanzania kuwahamasisha wanamichezo hao.
Michezo ya Jumuiya ya Madola inayotarajiwa kufunguliwa rasmi Jumatano (23 Julai 2014) na Malkia Elizabeth wa Pili itajumuisha nchi na Himaya 70. 
Michezo hiyo itafungwa tarehe 3 Agosti 2014. 

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI