Thursday, June 5, 2014

WIZARA YA UCHUKUZI YAADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA KWA KUFANYA USAFI NA KUPANDA MITI YA KUZUIA MMOMOMYOKO WA ARDHI KWENYE ENEO LA BANDARI YA DAR ES SALAAM LEO

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wizara ya Uchukuzi, Bw. Issa Nchasi, akifanya usafi katika eneo la bandari ya Dar es Salaam kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani ambayo kwa mwaka huu kauli mbiu ni ‘Tunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi Tanzania’.
Sehemu ya wafanyakazi wa Wizara ya Uchukuzi na taasisi zake wakiwa kwenye zoezi la usafi wa mazingira katika eneo la Bandari ya Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya Mazingiza Duniani.
Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira wa Wizara ya Uchukuzi, Bi, Tumpe Mwaijande (kulia), akipanda mti katika eneo la bandari ya Dar es Salaam leo asubuhi, kama sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Mazingira. Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira yanafanyika kitaifa mkoani Mwanza ambapo kwa mwaka huu kauli mbiu ni ‘Tunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi Tanzania’. (Picha na kitengo cha mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI