Thursday, June 5, 2014

UZUNGU WA WAZUNGU UKIPITILIZA, HAYA NDIO MATOKEO YAKE, WAJA NA KIPINDI CHA TV KUONYESHA WANAWAKE WAKIJIFUNGUA PORINI

birth
Kampuni ya Lifetime ya nchini Marekani imetangaza kipindi kipya cha Televisheni kitakachoonyesha wazazi vijana wakijifungua porini bila msaada wa madaktari wakati wa hatua zote za kujifungua lakini pia hawatakuwa na malazi yoyote katika eneo hilo.
birth2
Kipindi hicho “Born in the Wild” kitatoa taswira kwa wanawake na wanaume ambao wanaamini kuwa kujifunga mtoto katika mazingira mazuri na kupatiwa huduma zote mbali na madaktari ni njia pekee.
birth3
Kipindi hicho kimetokana na video iliyopata umaarufu mkubwa katika mtandao wa YouTube na kutazamwa mara milioni 20 ikionyesha mwanamke akijifungua porini lakini tayari wakosoaji wa mambo wanasema kipindi hicho kinaweza kutoa taswira ya kuhatarisha maisha ya wamama na watoto wanaopitia mazingira hayo

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI