Rapa wa muziki kutoka nchini Marekani Kanye West ameelezea wasiwasi wake juu ya usalama wa mtoto wake wa pekee North West katika macho ya jamii ambapo sasa anachukua hatua madhubuti katika kumlinda mtoto wake huyo wa kike kwa pamoja na mke wake Kim Kardashian.
Rapa huyo mwenye umri wa miaka 36 anadaiwa kuchukizwa na picha zote zilizopigwa za mtoto wake wakati wa kipindi cha harusi yake na Kim mwezi uliopita na anataka kuchukua tahadhari zaidi katika kumuweka salama mtoto wake huyo.
Kim na Kanye wamekuwa wakigombana juu ya jinsi mtoto wao North alivyowekwa hadharani wakati wa kipindi cha harusi.
Chanzo kimoja cha karibu na wanandoa hao kimesema kuwa Kanye hakujisikia vizuri jinsi mtoto wake alivyoonyeshwa sana hadharani na anataka kuhakikisha matukio kama hayo yanakwisha na anamlinda mtoto wake.
Kanye amekuwa mkali siku zote akipinga mtoto wake kupigwa picha hadharani lakini ameshindwa kulikabili suala hilo.
0 comments:
Post a Comment