Thursday, June 5, 2014

RIPOTI MPYA YA WALIOKUFA KUTOKANA NA EBOLA NCHINI GUINEA.

ebola
Umeshawahi kusikia kuhusu ugonjwa wa Ebola ambao umekuwa ukisumbua nchi kadhaa za Afrika na kusababisha vifo. Mpaka sasa takribani watu 208 wamepoteza maisha kutokana na virusi vya ugonjwa huo nchini Guinea kwa mujibu wa shirika la afya duniani.
Ripoti mpya iliyotolewa inaonyesha kuwa watu 21 wamekufa na watu 37 wamegundulika kupata virusi vya ugonjwa huo kati ya Mei 29 na June 1 mwaka huu na kufanya idadi kamili ya wagonjwa wa Ebola katika Ukanda wa Afrika Magharibi kufikia 328.
ebola2
Hakuna tiba wala kinga ya ugonjwa huo unaosababishwa na virusi hatari.
Zaidi ya nusu ya vifo vipya vilivyotokana na ugonjwa huo vimetokea katika Jimbo la Guekedou ambako ugonjwa huo umesambaa.
Watu watatu wamethibitishwa kupoteza maisha na wengine 10 kupata Virusi vya ugonjwa huo karibu na Sierra Leone na wengine 10 nchini Liberia.
Wataalamu wa afya wanasema moja ya sababu za kuongezeka kwa vifo ni kutokana na watu kukataa kwenda hospitali kwa ajili ya matibabu na kufuata tiba kwa waganga wa jadi.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI