HALI duni ya maisha huwalazimu watoto kufanya kazi hizo
Utumikishaji watoto katika migodi bado unaendelea nchini Tanzania licha ya serikali ya nchi hiyo kupiga marufuku utumikishwaji wa watoto.
Mererani mkoani Manyara, Kaskazini mwa Tanzania ni maarufu kwa uchimbaji wa madini aina tanzanite. Hata hivyo mgodi huo na hasa kwa wachimbaji wadogo bado tatizo la utumikishwaji linaendelea.
Mazingira ya uchimbaji madini ya Tanzanite yanaonekana ni ya hatari kwani inawalazimu wachimbaji mgodi kutumia shimo dogo la kipenyo cha takribani mita moja au mbili hivi kushuka kwenda chini ardhini kwa kutumia ngazi au kamba.
Mashimo haya ni marefu yanafikia takribani mita 300 na mengine hadi mita mia 800 toka usawa ardhi, ndani ni giza na hewa ni nzito na sura za wachimbaji mgodi hazitamaniki kwani ni wametapaa vumbi jeusi na nguo zao zimechafuka.
Sheria sio kizuizi
Watoto wa kati ya umri wa miaka 12 na 13 hutumikishwa katika migodi
Lakini hilo haliwazuii wachimbaji mgodi wakubwa kwa wadogo kuendelea kufanya kazi hiyo katika mazingira hayo.
Mbali na serikali ya Tanzania kupiga marufuku watoto kufanya kazi kwenye migodi lakini baadhi yao wanaokadiriwa kuwa na miaka kati ya 12 au 13 na wengine kati ya miaka 15 hadi 17 wanafanya kazi katika migodi mbali mbali ya wachimbaji wadogo eneo hilo la Mererani.
Baadhi ya watoto wamepoteza maisha na wengine wamekuwa wakiishi maisha ya tabu na hata kukosa chakula.
Tanzania ni miongoni mwa nchi 174 zilizoridhia azimio namba 182 la kukomesha utumikishaji watoto chini ya umri wa miaka 18.
Hata hivyo pamoja na jitihada za serikali ya nchi hii kujaribu kupiga vita utumikishaji watoto bado watoto wamekuwa wakitumikishwa.
0 comments:
Post a Comment