Friday, June 6, 2014

MMMMH! MHE. KOMBA!!?? AFUNGUKA YA MOYONI BAADA YA PICHA HIZI AKIWA NA BINTI CHUMBANI KUSAMBAA MITANDAONI!

komba2
Baada ya kusambaa kwa picha ambazo si nzuri katika mazingira ya kawaida zikimuonyesha Mhe. Kaptein Komba akiwa amepiga picha na msichana chumbani huku zikimuonyesha msichana huyo amevaa kanga na wakati mwingine bila kuwa na nguo kabisa kifuani (Picha hiyo haijawekwa kutokana na maadili).
Kuzungumzia tukio hilo moja kwa moja kutoka Dodoma Mhe. Komba anasema hajui kuhusiana na picha hizo kwani hajawahi kabisa kuwa katika mazingira hayo na binti huyo bali hao ni mtu ambaye amezitengeneza na hajui kwanini amefanya hivyo.
Mhe. Komba anasema “Picha nimewahi kupiga nyingi tangu utotoni lakini hizi za leo hata mimi zinaniogopesha, siwezi kuwa mwaguzi kujua nani amefanya hivyo lakini ukiangalia kuna roho ya uadui kati yangu mimi na huyo mtu ambaye ameamua kunifanyizia, kaamua kuingia vitani na anaweza kufanya hivyo kwa namna nyingi inaweza kuwa kisiasa au kiurafiki lakini zimenipa tabu sana, zimeisumbua familia yangu, marafiki zangu kwakweli zimenisumbua sana.”
KOMBA 1
Mhe. Komba anaendelea kwa kusema kuwa “Nimepokea simu nyingi sana mpaka nafunga simu kila anayepata anantakia mema, ni wachache wanaontukana lakini wengine wanantakia mema. Ukiangalia shingo si yangu, mwili si wangu yule binti mara akae uchi kwahiyo aliyetuma ana sababu zake na kama kweli mimi ningekuwa nafanya mambo hayo basi angezituma picha ambazo hata mimi niko uchi kama huyo mwanamke.”
“Mke wangu kanipigia simu kunipa pole, watoto wangu wote ni watu wazima wamepigia simu kunipa nguvu. Jamii imuogope Mungu mimi namwachia Mungu apigane na maadui zangu, usifanyie watu usiyotaka kutendewa.”
“Nikijua aliyenifanyia hivyo akija kwa kuniomba msamaha ntamsamehe lakini hili suala limeniathiri sana kisaikolojia hata bungeni leo sijaenda.”

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI