Monday, June 16, 2014

MASHAMBULIZI MAPYA KENYA, WATU 48 WAUWAWA

kenya1
SHIRIKA la habari la BBC limeripoti kuwa, Takribani watu 48 wameuwawa baada ya kikundi kinachodaiwa kuwa cha wapiganaji wa kiislamu kushambulia hoteli na kituo cha polisi katika mji wa Pwani wa nchi hiyo, kwa mujibu wa maafisa kutoka Kenya.
kenya2
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa walishuhudia mapigano ya risasi yaliyodumu kwa saa kadhaa pamoja na majengo kuchomwa moto.
Mji huo uko karibu na kisiwa cha Lamu ambacho ni maarufu kwa hoteli nzuri za kitalii.
LAMU
Kenya imekuwa ikikumbwa na mashambulizi ya kigaidi tangu mwaka 2011 wakati vikosi vyake vya kijeshi vilipoingia Somalia kwa ajili ya kusaidia kupambana na wapiganaji wa kikundi cha al-Shabab.

UNGANA NASI KWA KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI