Tuesday, June 17, 2014

KAMA HUJASIKIA ALICHOFANYA SHILOLE NA KUWAACHA MASHABIKI MDOMO WAZI, KWENYE KILITOUR HIKI HAPA..!

IMETOKEA kuwashangaza wengi sana kwa tukio hili la aina yake alilosababisha msanii wa Bongo fleva mwenye miondoko tofauti kabisa na ya HipHop, Story nzima ilikuwa hivi: 
Wakati mzee wa mitulinga maarufu kama Prof J alipokuwa anaperform huko mjini Songea kwenye Kili tour, mara ghafla shilole akavamia shoo na kuanza kuimba Nyimbo ya zali la mentali, aliyokuwa anaiimba Professor J, 
Jambo hili lilisababisha mashabiki wengi sana kupiga kelele za shangwe pale kati wakimshangilia mwanadada huyo na kuwaacha wengine midomo wazi wa kutoamini kwa tukio hilo lililotokea.
Hii inaonyesha kukubalika sana kwa mkongwe huyu hata na wasanii wenzake, na wengine kushindwa kujizuia kupiga shangwe hasa pale akikumbushia nyimbo zake zilizowahi ku-make headlines enzi za mwalimu.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI