Monday, June 23, 2014

'DIAMOND' SUKARI YA WAREMBO, ATHIBITISHA KWA LIST HII YA WANAWAKE ALIOWAHI KUWA NAO!

WALIOSEMA ujana ni maji ya moto hawakukosea. Mkali wao kwenye Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ni msanii ambaye ana idadi kubwa ya msururu wa wanawake ambao ametoka nao kimapenzi ambapo, wapo wanaojulikana na wengine hawajulikani.
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
LEO katika makala haya tunakuletea wanawake ambao kwa nyakati tofauti walibanjuka kimapenzi na Diamond ambao kimsingi kutokana na idadi yake, anadhihirisha jina lake la Sukari ya Warembo.
Takwimu zinaonesha kuwa karibu kila mwaka jamaa anabadilisha wapenzi ambapo wanawake wamekuwa wakipokezana vijiti.
*************
UPENDO MUSHI ‘PENDO’
Huyu ni msanii wa filamu ambaye alitokea katika Shindano la Maisha Plus. Aliwahi kukiri kwamba alishatoka kimapenzi na Diamond kabla hajawa maarufu kama alivyo sasa, hawakudumu muda mrefu.
****************

WEMA SEPETU
Ni mlimbwende wa Tanzania na msanii wa filamu kwa sasa. Diamond baada ya kupata umaarufu kidogo, alikutana na Wema na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi jambo lililofanya umaarufu wake kuzidi mara dufu.

Wema na Diamond waliachana na kila mmoja akawa anaendelea na maisha yake lakini mwaka jana wawili hao walirudiana na mpaka sasa wapo pamoja. 
*******************
PENNIEL MUNGILWA ‘PENNY’ 
Kwa muda huo ambao Diamond aliachana na Wema, ulikuwa ni mwanya wa Mtangazaji wa Runinga ya DTV, Penniel Mungilwa kumiliki penzi la Mbongo Fleva huyo.
Alikuwa ni rafiki wa karibu na Wema, akampindua kwa Diamond. Mapenzi yao yalidumu kwa muda mfupi kabla ya mkali huyo kurudisha majeshi kwa Wema kwa mara nyingine.
*****************
ANGEL MAGGY
Diamond wakati akiwa na Wema kabla hawajaachana iliripotiwa kwamba alikuwa akisaliti penzi lao ambapo alitoka kimapenzi na msichana Angel ambaye ni Mkenya lakini hawakukaa muda mrefu, wakamwagana. 
******************
JOKATE MWEGELO 'KIDOTI'
Ni mwanamitindo maarufu Tanzania. Penzi lao lilikuwa la muda mfupi na la siri kwani hawakujiachia kama ilivyokuwa kwa Penny na Wema.
Huyu naye alikuwa ni rafiki wa Wema lakini alitoka naye kimapenzi ambapo baada ya kuachana, Diamond alimuomba msamaha na kusema alimkosea sana kwani ni mwanamke ambaye alimpenda lakini alimpotezea baada ya kumpata Wema. 
Na huyu ndiye alidaiwa na Wema kwamba aliingilia penzi la ‘sukari wake’. Alimtuhumu kutoka na Diamond, ikawa uhasama mitaani  na 
habari ya mjini kwa wakati huo ikawa Wema, Diamond na Jokate.
Jokate amekuwa akikana kutoka na Diamond japo ushahidi wa kimazingira upo, Diamond awali alikataa, kuna siku akakiri.
*******************
JACQUELINE WOLPER
Kama ilivyoandikwa awali, alidaiwa kutoka na Diamond wakati hana jina kubwa kama alivyo sasa. Walipotafutwa wote, Diamond
alikanusha, Wolper pia aliruka kimanga, lakini watu wa karibu yao waliitaja hata hoteli waliyokuwa wakikutana, ipo Magomeni Kagera, Dar.
Inasemekana kuwa Wolper na Diamond walitoka kimapenzi lakini waliachana katika mazingira ya kutatanisha jambo lililomfanya Diamond amtungie wimbo kutokana na jinsi alivyoumia.
********************
NAIMA 
Huyu alikuwa ni rafiki wa karibu sana wa Wema lakini alitoka kimapenzi na Diamond hali iliyosababisha wanawake hawa kuwa na bifu kwa sababu ya kushea mwanaume huyo mmoja.
****************
REHEMA FABIAN
Huyu ni mrembo aliyeshikilia Taji la Miss Kiswahili ambapo naye aliingia kwenye listi ya kutoka kimapenzi na Diamond. Uhusiano wa wawili hawa haukuwa wa muda mrefu ilikuwa ni kama kupita tu. Walipotafutwa kwa simu, Rehema alikiri lakini Diamond alichomoa akidai wanafahamiana.
******************

NATASHA
Huyu mrembo ameshaonekana kwenye moja ya video za Diamond katika wimbo wa Moyo Wangu. Aliwahi kuingia kwenye bifu na
Wema Sepetu akituhumiwa kutoka na msanii huyo wa Bongo Fleva. Mwenyewe alikiri kwa mapaparazi, lakini Diamond kama kawaida
yake, akachomoa.
**************
NELLY KAMWELU
Ni mwanamitindo maarufu hapa Bongo, na ametokea kwenye video kadhaa za wanamuziki maarufu ilidaiwa wawili hao kuna kitu ndani yake, hasa kinachohusu mahaba. Wadadisi wa mambo wakabaini ukweli wa madai hayo kwa nguvu za picha ambazo zinawaonyesha wawili hao wakiwa katika mapozi mbalimbali ya kimahaba.
“Kwa sasa Diamond yuko juu sana, imefikia hatua anawapanga foleni mademu kwa sababu wengi wao wanataka kuwa na kijana maarufu kama yeye,” alisema mmoja wa waliozishuhudia picha hizo.
MAHOJIANO NA WAWILI HAO...
Nilipopitia katika mtandao nkagundua AMANI walishawahi kufanya naye intavyu, ifuatilie nukuu hiyo hapa:
Amani baada ya kujiridhisha kwa Diamond ‘kuwapitia’ mastaa hao, achilia mbali wale wa ‘mechi’ za mchangani, lilimtafuta Nelly ili
kumpa haki yake ya kujieleza kuhusu madai hayo, akafunguka:
“Haaaa! Jamani! Kweli kwa siku hizi nipo karibu sana na Diamond, kwa sababu namsaidia mambo kibao wakati akiandaa video ya
wimbo wake mpya (Nataka  kulewa), nikawa napiga naye picha mbalimbali ambazo nilizipost BBM.
“Lakini hakuna sehemu yoyote niliyowahi kumtaja Diamond ni mpenzi wangu, ila nilijua watu watakuja kuzusha kuwa natoka naye
ndiyo kama hivi sasa.
“Mimi nina mchumba wangu hata Diamond anamjua na nipo naye kwa zaidi ya miaka sita sasa ingawa hivi karibuni tulikuwa na
matatizo ambayo tayari tumeshayamaliza. Diamond ni rafiki tu. Lakini kama ishu ipo kwenye kupiga picha, mbona akina Najma,
Wema, Jokate wameshapiga picha na Diamond?”
Kwa upande wake Diamond, alipopatikana kwenye simu na kuulizwa kuhusu Nelly, alitoa sauti yenye maneno haya:
“Nelly kwa sasa ni zaidi ya dada yangu maana kuna mambo kibao ananisaidia kwenye ‘shooting’ ya video ya wimbo wangu mpya,
nilimuomba anisaidie kwa kuwa ana uzoefu wa mambo ya mitindo. “Sina uhusiano naye zaidi ya kazi na urafiki wa kawaida ambao mtu
yeyote anaweza kuwa nao.”
*******************
AUNT EZEKIEL
Huyu mdada ambaye sasa ni mke wa mtu, yeye aliwahi kudaiwa kulala na Diamond kwenye hoteli moja maarufu mitaa ya Bamaga,
Dar. Walipotafutwa, Aunt alikiri kuwepo kwenye hoteli hiyo akisema alikuwa na mpenzi wake ambaye ni rafiki wa Diamond.
Diamond pia alikiri kuwepo kwenye hoteli hiyo, lakini akasema alimfuata rafiki yake ambaye ndiye mpenzi wa Aunt! watu wanabaki Mmmmh!
*****************
NUZLAH A-BOUBAKAR
Katika ziara yake ya kimuziki Mombasa, Kenya, Diamond alikutana na huyu mrembo.  Picha za wawili hao wakiwa kwenye pozi la 
kimahaba zikasambaa mtandaoni. 
Wakadaiwa ni wapenzi lakini Diamond akashindwa kutoa maelezo yanayojitosheleza kuhusu madai hayo.
*************
DIAMOND KWA SASA YUPO HAPA!!! 
Baada ya sarakasi zote za wapenzi, sasa Diamond ametulia kwa Beautiful Onyinye, Wema Sepetu ambaye amekuwa na Diamond kwa miaka miwili sasa ila mapenzi yao yako hivi; wanaachana, wanarudiana, wanaachana wanarudiana.
Kwa sisi wapenzi wa muvi na bongo fleva sisi yetu macho…. Kikubwa ni burudani wanayotupa ili mengine mmmh tuwaachie wenyewe maisha yao.
Ni hayo tu kwa leo.
Tuandikie kwa lolote ulilonalo mdau wetu wa mtandao huu wa ULIMWENGU WA HABARI

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI