KATIKA kusherekea uhuru wake mwanamuziki maarufu nchini marekani Chriss Brown anatarajia kufanya sherehe kubwa kwaajili ya kusherekea na marafiki zake maarufu kwa kuwa free, nje ya kitengo (Jela).
Wasanii kama Akon, Amber Rose, Big Sean, Tyga, T-Pain na Karrueche Tran walikuwa ni kati ya watu muhimu waliohudhulia katika chumba maalumu hapo tar 05/06/2014 (Alhamis) baada ya mwanamuziki huyo kuachiliwa huru!
'Katika chumba hicho kulikuwa na muziki kiasi na baadhi ya watu walionekana wakipata msosi wa hapa na pale, Chris Brown alipoingia huku akionekana ni mtu aliyetulia na mwenye afya tele, watu wote walisimama na kugonga cheers, kama ishara ya kumpokea mwanamuziki huyo', Kiliripoti chanzo kimoja.
Chriss Breezy aliachiwa huru kutoka katika gereza la Los Angels mida ya saa sita na dk 1 mchana siku ya Jumatatu ambapo alitumikia kifungo cha zaidi ya miezi miwili baada ya kutokuwa na nidhamu katika kipindi cha kuangaliwa tabia baada ya kuhusika na kesi ya kumpiga mpenzi wake wa zamani Rihanna, na ataendelea kuripoti kwa afisa wa polisi aliyepangiwa kujua mabadiliko ya tabia yake hadi itakapofika tar 23, 2015.