Saturday, June 7, 2014

CHATU LILILOKUTWA LIKIRUDI NDANI YA NYUMBA YA MFANYABIASHARA MAARUFU WA JIJINI ARUSHA LAUAWA NA WANANCHI

Joka hilo kubwa aina ya Chatu likiwa nje ya Nyumba ya mfanyabiashara huyo, ambalo lilikutwa likiwa limefungwa Kitambaa cheupe kilichokuwa na maandishi ya Kiarabu, ambapo wananchi wamefananisha suala hilo na imani za kishirikina. Joka hilo baada ya kudhibitiwa liliburuzwa hadi katika Kanisa Katoliki la Karsamatiki lililopo eneo la Sakina jijini Arusha na kuanza kuuawa na wananchi.
Chatu huyo akiburuzwa kuelekea kucharangwa baada ya kuuawa.
Jamaa akiendelea na zoezi la kumcharanga chatu huyo.
Nyumba ya mfanyabiashara maarufu wa jijini Arusha, aliyetambulika kwa jina la Joseph Magese, alikotolewa nyoka huyo aina ya Chatu na kuuawa na wananchi kwa kucharangwa mapanga.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI