RAIS mpya wa Misri, Abdel-Fattah al-Sisi, amesema kuwa atakuwa kiongozi wa raia wote wa Misri, lakini akaapa kuwa hatapatana na kundi lililopigwa marufuku la Muslim Brotherhood.
Katika hotuba yake ya kwanza kwa taifa, Bwa Sisi alisema kuwa jambo atakalolitilia mkazo kwanza ni kupambana na ugaidi na kurejesha amani.
Alipokuwa mkuu wa jeshi alimpindua kiongozi wa Kiislamu aliyekuwa amechaguliwa, Mohammed Morsi, Julai na kutangaza kuwa kundi la Muslim Brotherhood ni la kigaidi.
Katika hotuba yake aliahidi kuimarisha hali ya maisha ya wananchi wa Misri.
Hata hivyo alionya kwamba uhuru lazima uende sambamba na nidhamu.
Mwandishi wa BBC mjini Cairo amesema kuwa wapinzani wa Bwana Sisi wana hofu kuwa utawala wake wa miaka minne utakuwa wa kiimla.
0 comments:
Post a Comment