Friday, May 2, 2014

MAMA SALMA KIKWETE MGENI RASMI MAADHIMISHO YA SIKU YA WAKUNGA DUNIANI

MKE wa Rais, Mama Salma Kikwete, anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani, zinazotarajia kufanyika Mei 5, jijini Dar es Salaam. 
 Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) kitaadhimisha   siku ya Wakunga Duniani   (International Day of Midwives hapa nchini kwa siku mbili kuanzia tarehe 4hadi 5/2015.  

      Siku ya Wakunga Duniani huadhimishwa duniani kote tarehe tano mwezi wa tano ya  kila mwaka. 
Madhumuni ya Maadhimisho hayo ni kuhamasisha  Wadau mbalimbali  pamoja na Jamii kwa ujumla  kuhusu umuhimu wa wakunga na shughuli  wanazozifanya katika kupunguza vifo vya  akina mama vinavyotokana na uzazi pamoja na vifo  vya  watoto wachanga na wenye umri chini ya miaka mitano.
Kauli Mbiu ya Mwaka huu (2014) ni “Wakunga Wataalam Wanahitajika Duniani kwa wingi sasa kuliko siku zote.” (The World Needs Midwives Today Than Ever)   
Hii inalenga katika  kuhakikisha kuwa huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto zinatolewa na Wakunga wenye utalaam kwa kufuata  miongozo na viwango vilivyowekwa   ili  kuchangia katika   kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia  namba  3,4, 5 na 6.  
Tanzania ni mmojawapo ya  nchi   zenye uhaba  wa  watao  huduma wenye ujuzi hususani Wakunga  katika ngazi ya  zahanati na vituo vya afya ambako ndiko wakinana  mama wengi wanapata huduma ya  wakiwa wajawazito, kujifungua na baada ya kujifungua.  

TANZANIA MIDWIVES ASSOCIATION  (TAMA)  
Address: HQ Dar Es Salaam   
P.O. Box 65524 Dar Es  Salaam Tanzania E-Mail: seolesh@yahoo.com  
Katika kuadhimisha siku hiyo, Wakunga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali   watafanya shughili tatu ambazo ni:  
1. Kongamano la kisayansi kwa   siku moja tarehe 4/5/2014   ambapo watajadili   mada  na shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wakunga.  
Mahali :   Hospitali ya Taifa ya Muhimhili  Jengo la  New  OPD  Chumba no 60,   linaloangaliana na Wadi ya Wazazi  
Mgeni Rasmi: Mheshimiwa Dkt. Seif S Rashidi (MB)  Waziri wa Afya na Ustawi Wa Jamii  
2 Kutoa huduma  za afya ya uzazi na mtoto katika viwanja vya Mnazimmoja kwa akina mama, watoto , vijana na wanaume kwa siku mbili 4/hadi 5/2014. Huduma zitakazotolewa ni:  
* Uzazi wa mpango,  
* Chanjo kwa watoto  
* Ushauri na upimaji  wa hiari  wa virus vya UKIMWI, 
 * Uchunguzi wa saratani ya  matiti na kizazi kwa akina mama
* Utoaji  wa hiari wa damu.  
* Elimu na   ushauri kuhusu hudma ya Afya ya Uzazi na Mtoto 
* Wanaume watapata sindano ya Pepopunda ( tetanus)  
Huduma zitakazotolewa ni bure hakuna malipo.   
3 Kufanya mandamano kutoka makao makuu ya Wizara ya Afya  hadi Viwanja vya Mnazimmoja siku ya kilele tarehe 5/5/2014. Maandamano yataongozwa na Brass band ya JKT Mgulani. 
         Mgeni Rasmi ni:  Mheshimiwa Mama Salma Kikwete, Mke wa Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  
Kwa heshima na taadhima Chama kinaomba vyombo vya habari kutusaidia  kutoa taarifa kwa  Wananchi.  
Tunatanguliza shukurani zetu.
    
Dr Sebalda Leshabari
 KATIBU MKUU TAMA

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI