Wednesday, May 21, 2014

KATIBA MPYA TUNAITAKA,LAKINI ISIWE YA KUKOROGA VICHWA VYA WATU - KATIBU MKUU WA CCM, KINANA

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua nyumba hiyo ya zamani iliyokuwa inatumiwa na Mfugaji Mihangwa, kabla ya kujenga nyumba ya kisasa katika Kijiji cha Heka, wilayani Manyoni, Singida.
Kinana akiangalia mifungo ya Mfugaji Mihangwa iliyobakia baada ya kuuza mingine kwa ajili ya kujenga nyumba ya kisasa.
Mihangwa anasema aliamua kuuza ng'ombe 200 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo ya kisasa.
Kinana akizindua nyumba Mfugaji huyo ya kisasa kabisa . Kulia ni Mfugaji Mihangwa mmiliki wa nyumba hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (haonekani pichani) na wajumbe wengine wakitoka nje ya nyumba ya kisasa ya Mfugaji Mihangwa mara baada ya kuikagua,Bwan.;Mihangwa aliuza ng'ombe zake 200 na kubaki na ng'ombe 100 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo ya kisasa kama ionekanavyo pichani. 
jengo la maabara ya Shule ya Sekondari Heka kama lionekanavyo pichani
Kinana akisaidia kumpatia tofali fundi wa jengo la maabara ya Shule ya Sekondari Heka wakati wa ziara yake katika Jimbo ya Manyoni Mashariki. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki, Kapteni John Chiligat 
Kinana akilakiwa na mabango katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Heka wakati wa ziara yake wilayani Manyoni. 
Nape akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Heka, ambapo aliwaambia wananchi kuwapuuza wapinzani kwani hata wakifanya mkutano hawasaidii wananchi katika masuala ya maendelo, bali wamebaki wakihubiri suala ya Katiba Mpya.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimtambulisha Mbunge wa jimbo la Manyoni Mashariki,Kapt.John Chiligati kwa wananchi wa Kijiji cha Heka katika mkutano wa hadhara.Aidha Mh.Chiligati alielezea katika mkutano huo miradi mbalimbali iliyotekelezwa katika eneo hilo la Heka.
Wanachama wapya wakila kiapo ha utii cha CCM baada ya kujiunga na chama hicho katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Heka, Manyoni.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki mazoezi ya Wanafanzi walioko kambini kwa ajili ya mashindano ya UMISSETA wilaya ya Manyoni jioni ya leo mkoani Singida.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akihutubia kwenye mkutano wa hadhara ambao pia ulihudhuriwa na Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika Stendi ya Manyoni, willayani Manyoni, Singida leo. Nape amesema kitendo cha vyama vya upinzani kuunda Ukawa umekirahisishia CCM kuvishambulia vyama hivyo kwa pamoja badala ya kimoja kimoja.
Sehemu ya umati wa watu wakifuatulia yaliyokuwa yakizungumzwa uwanjani hapo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia kwenye mkutano wa hadhara katika Stendi ya Manyoni, wllayani Manyoni, Singida leo. "Katiba tunaitaka, lakini isiwe ya mazingaombwe ya kukoroga vichwa vya watu. ndugu msitoane macho, tusing'oane meno kwa ajili ya katiba ambayo hata ikija mpya haiwezi kugeuza chai ya rangi kuwa ya maziwa" alisema Kinana akatika mkutano huo.. 
Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki, Kapteni John Chiligati akiwahutubi wananchi wa mji wa Manyoni mapema leo kwenye stendi ya mabasi Manyoni.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Stendi ya Manyoni, wllayani Manyoni, Singida leo. "Katiba tunaitaka, lakini isiwe ya mazingaombwe ya kukoroga vichwa vya watu. 
Ndugu msitoane macho, tusing'oane meno kwa ajili ya katiba ambayo hata ikija mpya haiwezi kugeuza chai ya rangi kuwa ya maziwa" alisema Kinana akatika mkutano huo.Ndugu Kinana yupo mkoani humo kwa ziara ya siku 8 akitokea mkoani Tabora ambako alikuwa na ziara ya siku 11.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI