Tuesday, April 22, 2014

VAN GAAL APEWA NAFASI YA KUCHUKUA KITI CHA MOYES

Louis Van Gaal ndiye anayepewa nafasi kubwa zaidi ya kuchukua nafasi ya Kocha David ‘Daudi’ Moyes wa Man United.
Van Gaal anaelezwa kuwa na urafiki wa karibu zaidi na mshambuliaji Robin van Persie aliyewahi kumfundisha kwenye timu ya taifa ya Uholanzi.


Moyes amekuwa katika wakati mgumu katika hatua za mwisho za Premiership baada ya kupoteza mechi 11 za ligi hiyo.
Tokea ametua Man United akitokea Everton, mambo yanaonekana kumuendea vibaya na taarifa zinasema viongozi wa Man United wameonyesha kuchoshwa naye.

VAN GAAL:
Klabu alizofundisha
Ajax, 
Barcelona, 
AZ Alkmaar, 
Bayern Munich

Timu ya taifa aliyofundisha
Uholanzi

Makombe akiwa na klabu
                   Ubingwa wa ligi                   7
                   Ligi ya Mabingwa                 1
                   Kombe la UEFA                    1
                   Makombe ya kawaida          7
                    Makombe mengine Ulaya    3 

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI