
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete
akiwapungia mkono wananchi
waliohudhuria sherehe za miaka 50
ya Muungano wa Tanganyika
na Zanzibar zilizofanyika kwenye
uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam
na kuhudhuriwa na Viongozi
mbali mbali wa ndani na nje ya nchi.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua
gwaride la Jeshi la wananchi kwenye sherehe
za miaka 50 ya Muungano wa Tanzania.

Kikosi cha Makomandoo kikipita kwa
mwendo wa aina yake wakati wa sherehe
za miaka 50 ya Muungano.

Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Muungano ambazo zimefanyika katika Uwanja wa Uhuru
jijini Dar es salaam.

Kikosi cha Makomandoo kikitoa salaam
kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania katika sherehe za kuadhimisha
miaka 50 ya Muungano.

Makomandoo wakionyesha namna ya
kupambana bila kutumia nyenzo hapa
wakivunja matofali kwa kutumia kichwa
na mikono.

Baadhi ya silaha zakijeshi zikipitishwa
mbele ya umati kuonyesha uwezo mkubwa
wa jeshi letu.

Kikosi cha Wanamaji

Ndege za kivita zikilinda Ndege ya Rais
katika maonyesho ya Ndege yaliofanyika
kwenye Kilele cha Maadhimisho ya miaka
50 ya Muungano.

Askari wa kikosi cha Mwamvuli akishuka
kutoka futi 4500 kwenye uwanja wa Uhuru
kwenye kilele cha miaka 50.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa mkono
wa pongezi mmoja wa wanajeshi wa
kikosi cha mwamvuli .

Maandamano ya Pikipiki.

Matembezi maalum ya kusheherekea miaka
50 ya Muungano .

Njiwa wakirushwa juu kama ishara ya
miaka 50 ya Muungano ambapo watu
waliorusha njiwa hao nao wametimiza
miaka 50.
0 comments:
Post a Comment