Wednesday, April 2, 2014

KAMATI ZA BUNGE ZA BUNGE MAALUM ZAANZA KAZI VIZURI

Na Magreth Kinabo – Dodoma
KAMATI 12 za Bunge Maalum zimeaanza kazi vizuri ya kuchambua Rasimu ya Katiba, huku baadhi ya wenyeviti wakisema kuwa muda wa siku mbili wa kujadili sura ya kwanza na ya sita hautoshi.
Hayo yamebainika katika mahojiano ya Mwenyekiti wa Kamati namba 11 ya Bunge hilo, Anne Kilango Malecela, yayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa St. Gasper mjini Dodoma.
“Tatizo lililojitokeza ni kwamba muda wa siku mbili hautoshelezi , leo tumejadili sura ya kwanza sehemu ya kwanza kesho tutajadili sehemu ya pili ya sura ya kwanza hivyo tunaweza tusiiguse sura ya sita.
“Wenzetu walikakataa Kanuni zisirekebishwe. Lakini wenzetu wapinzani wameliona hilo wameanza kusema muda hautoshi,” alisema Anna .
Ameongeza kuwa kutokana na hali hiyo atamweleza Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samwel Sitaa (leo jioni ) kuwa muda hautoshi.
Mwenyekiti huyo tatizo lingine lililojitokeza katika kamati yake ni baadhi ya wajumbe kutokuwa na uelewa wa tofauti ya dola na nchi, hali iliyomfanya kutumia kanuni namba 56(7) kumwomba Mwenyekiti wa Bunge hilo ikiwezekana kumleta mtaalamu wa sheria ili kuweza kutoa elimu hiyo leo (jioni) juu ya masula hayo.
Akizungumzia kuhusu mjadala alisema wajumbe wote walijitayarisha vizuri na walishindana kwa hoja hivyo hakuna aliyetoa maneneo makali.
Akizungumza kwa njia ya simu na waandishi wa habari nje ya ukumbi huo, kwa sababu alikuwa katika Mwenyekiti wa Kamati namba moja, Ummy Ali Mwalimu alisema wajumbe walichangia kwa utulivu.
Ummy alisema kilichojitokeza katika kamati yake ni kuwa muda hautoshi kama ilivyodaiwa na baadhiya wajumbe kutoka upinzani, chama tawala na kutoka 201.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya namba tano ya Bunge hilo, Hamad Rashid alisema kamati yake mjadala unaendelea vizuri na ulikuwa wa kistaarabu.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI