Thursday, April 10, 2014

GARI LANGUA MAENEO YA SALENDER BRIDGE

Gari aina ya RAV 4 ambayo haikuweza kufahamika mara moja namba za usajili kutokana na mmiliki wake baada ya ajali hiyo hakuweza kuongea lolote zaidi ya kulia... limeteketea kwa moto jana Aprili 9, 2014 katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa waliona watu wakikimbia ovyo baada ya kutanda kwa moshi mkali na baadae waliona moto ukizuka ila inaonekana chanzo cha ajali hiyo ni hitrafu ya umeme kwenye gari hilo.
Katika ajali hiyo hakuna mtu aliyefariki wala kujeruhiwa. 
Mabaki ya gari hiyo...
Muonekanao wa gari hilo kwa nyuma.
Mashuhuda wa ajali hiyo wakiwa eneo la tukio.
Picha na Kajuna son

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI