Monday, March 17, 2014

USHINDI WA ASILIMIA 79.4 WA CCM DHIDI YA CHADEMA KALENGA HUU HAPA

Wanachama na wapenzi wa CCM kalenga wakiwa wamembeba mshindi wa kiti cha ubunge jimboni humo Bw. Godfrey Mgimwa.


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka kidedea katika uchaguzi wa kumpata Mbunge wa jimbo la Kalenga, baada ya kuzoa kura kwa asilimia 79.4 dhidi ya wapinzani wao Chadema waliopata asilimia 20.1 na Chausta 0.51.

Kwa nafasi hiyo, Mgombea wa CCM Godfrey Mgimwa amekuwa Mbunge mpya akichukua nafasi ya Mbunge aliyefariki jimboni humo, Dr William Mgimwa.

Matokeo ya uchaguzi huo, yanatoa nafasi nyingine kwa CCM kuweka rekodi ya kushinda chaguzi ndogo za ubunge katika majimbo mbalimbali yaliyokuwa nyameachwa wazi.

Kwa mujibu wa matokeo hayo, CCM imeshinda kwa kura 22,943 dhidi ya kura 5,800 za Chadema huku chausta ikiambulia 143.

Ushindi wa jimbo la Kalenga, ni mwanzo wa kuanza mbio nyingine za uchaguzi katika jimbo la Chalinze

MATOKEO YA JUMLA KALENGA:

CCM wamepata Kura 22908 

CHADEMA Wamepata Kura 5800 

CHAUSTA kura 143.

CCM imeshinda kwa asilimia 79.4 

Chadema kwa Asilimia 20.1 

Chausta Kwa Asilimia 0.5


0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI