Monday, April 7, 2014

COCA-COLA YAZINDUA KAMPENI YA BRAZIL

-Kupeleka kumi na nne Brazil 
-Wateja kujishindia luninga za kisasa 1000 
-Mashabiki kutazama mechi za Kombe la Dunia bure kwenye luninga kubwa 
Meneja bidhaa wa Coca-Cola Tanzania Maurice Njowoka Meneja akiongea na waandishi wa habari wakati uzinduzi wa promosheni ya miezi miwili ya Kombe la FIFA la Dunia 2014, kushoto ni Meneja Mkazi wa Coca-Cola Tanzania Yebeltal Getachew. Hafla hiyo ilifanyika leo, Aprili 7 2014, jijini Dar-es-Salaam.
Meneja bidhaa wa Coca-Cola Tanzania Maurice Njowoka Meneja akiongea na waandishi wa habari katika uzinduzi wa promotion ya miezi miwili ya Kombe la FIFA la Dunia 2014, kulia ni Meneja mkazi wa Coca-Cola Tanzania Yebeltal Getachew. Hafla hiyo ilifanyika leo, Aprili 7 2014, jijini Dar-es-Salaam.
Meneja mkazi wa Coca-Cola Tanzania Yebeltal Getachew akiongea na waandishi wa habari katika uzinduzi wa promotion ya miezi miwili ya Kombe la FIFA la Dunia 2014, kushoto ni meneja bidhaa wa Coca-Cola Tanzania Maurice Njowoka. Hafla hiyo ilifanyika leo, Aprili 7 2014, jijini Dar-es-Salaam.

Kampuni ya Coca-Cola leo imezindua promosheni ya miezi miwili ya Kombe la FIFA la Dunia 2014 ambapo wateja wake watajinyakulia zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na tiketi za kwenda kushuhudia mchezo wa robo fainali wa Kombe la Dunia nchini Brazil. Zawadi nyingine ni pamoja luninga, mipira na fulana.“Mbali na wateja kumi na nne kupata nafasi ya kwenda Brazil, tunatatoa luninga 1000 za kisasa aina ya Sony LED zenye ukubwa wa inchi 32, mipira 8,000 yenye nembo ya FIFA World Cup na T-shirt 30,000”, Anasema Meneja Mkazi Coca-Cola Tanzania Yebeltal Getachew. Getachew alisema kuwa shindano hili la Kombe la FIFA la Dunia ni nafasi nyingine kwa Kampuni ya Coca-Cola kuweza kutoa sehemu ya mapato yake kwa jamii inayofanyia biashara na kupata fursa ya kuweza kuwa karibu na wateja wake.
‘Kombe FIFA la Dunia ndio mchezo wenye mashabiki wengi zaidi duniani. Kwa kushirikisha wateja wetu katika promosheni hii, Coca-Cola itawawezesha mashabiki wa soka nchini Tanzania kuungana na wengine duniani kote kusherehekea kwa pamoja burudani ya Kombe la Dunia 2014,’ anasema Getachew.Getachew alisema promotion hii itaendeshwa na kampuni za uzalishaji wa vinywaji vya jamii ya Coca-Cola: Nyanza Bottlers ambayo inahudumia Kanda ya Ziwa na Magharibi mwa Tanzania, Bonite Bottlers inayohudumia Kaskazini na Kanda ya Kati na Coca-Cola Kwanza inayohudumia sehemu zilizobaki pamoja na Zanzibar.Washindi watapatikana kwa kunywa vinywaji vya Coca-Cola na kupata vizibo viwili vyenye kutengeneza neno Brazil pamoja na kizibo cha ushindi. Kizibo cha ushindi kina picha ya kitu ambacho mteja ameshinda (TV, Mpira au T-shirt) wakati kizibo cha ushindi wa zawadi ya tiketi kina nembo ya ndege kikiashiria safari ya kwenda Brazili kushuhudia moja kwa moja mechi ya Kombe la Dunia, aliongeza Meneja Bidhaa Coca-Cola Tanzania Maurice Njowoka.Coca-Cola pia itaandaa sehemu za kuonyesha mechi za Kombe la Dunia bure kwenye TV kubwa hapa jijini Dar es Salaam na sehemu nyingine za mikoani. Kampuni ya Coca-Cola ni mshirika wa FIFA kwa muda mrefu, ambapo uhusiano rasmi ulianza tangu 1974 na kuwa mdhamini rasmi wa michuano ya Kombe la Dunia 1978. Coca-Cola imekuwa na matangazo kwenye viwanja vinavyochezewa michuano ya Kombe la Dunia tangu 1950. Novemba 2005, Coca-Cola na FIFA waliboresha mahusiano yao. Uhusiano huu unatazamiwa kuendelea hadi 2022, na kuuboresha zaidi kulingana na makubaliano yao.Kama mshirika wa FIFA wa kwa upande wa vinywaji baridi, Kampuni ya Coca-Cola ndio mwenye haki za mashindano yote ya FIFA, pamoja na ziara ya Kombe la Dunia.

Picha na Cuthbert Lucas

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI