Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Benard Membe (kushoto) akitoa ufafanuzi juu ya kazi mbalimbali zifanywazo na Wizara yake katika kulinda na kutengeneza amani ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Kulia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi J. Maalim. Mazungumzo hayo na Waandishi wa habari yamefanyika leo katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanahabari waliohudhiria mkutano wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Benard Membe wakati akielezea kazi mbalimbali zifanywazo na Wizara yake katika kulinda na kutengeneza amani ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Mazungumzo hayo na Waandishi wa habari yamefanyika leo katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa jijini Dar es Salaam.
Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Benard Membe afanya mazungumzo na waandishi wa habari juu ya ushirika wa Tanzania katika kulinda na kutengenza amani ndani na nje ya mipaka yake.
Mhe. Membe ametoa ameyasema hayo leo wakati alipofanya Mkutano na waandishi wa habari kuelezea juu ya kazi mbalimbali ambayo Wizara yake imekuwa ikifanya hasa ya kulinda na kutengeneza amani nchini.
Mhe. Membe amesema kuwa Wizara yake imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kutatua migogoro mbalimbali ikiwemo ya mipaka kati ya Tanzania na nchi jirani. Aidha, ametoa pongezi kwa vikosi maalum vya kulinda amani kwa kazi kubwa vinavyofanya katika kudumisha amani .
Waziri Membe amezungumzia pia juu kazi nyingine zifanywazo na Wizara yake hasa ktika kutafuta wawekezaji nje ya nchi ili kuja kuwekeza nchini ili kuinuna uchumi wa Tanzania ambapo imeweza kuvutia wawekezaji kutoka nchi mbalimbali ikiwemo nchi za China na Ujerumani . Aidha, ameongeza kuwa Wizara yake imeweza kuvutia nchi mbalimbali kufanya maombi ya kuanzisha balozi zao hapa nchini.
“Wizara imejitahid kwa kiasi kikubwa kuvutia mambio mbalimbali na mpaka hivi sasa kuna maombi yapatayo kumi toka kwa nchi mbalimbali zikitaka kuanzisha balozi zao hapa nchini kama vile Austarlia, Comoro na nyinginezo”. Alisema Waziri Membe.
Kwa upande mwingine Mhe. Membe alitaja moja ya changamoto inayokumbwa na Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo ni ya ukosefu wa viwanja vyenye viwango kwaajili ya kufanyia mafunzo kwa wanamichezo na hivyo amesema kuwa Wizara yake inajitahidi kuisaidia Wizara hiyo katika katika kutafuta maeneo nje ya nchi ili wanamichezo wapate kwenda kufanya mazoezi na kupata mafunzo.
“Mpaka hivi sasa tumepokea barua zipatazo kumi za kukubaliwa maombi kwaajili ya wanariadha wetu kwenda kufanya mazoezi na kupata mafunzo mbalimbali ambapo watu wapatao sitini wanatarajia kwenda nchini Newsland pamoja na nchi nyingine kama vile China na Uturuki wakiwemo Makocha kumi na sita hivo, Wizara yangu itashirikiana kwa karibu na Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo katika kwa ukaribu zaidi”. Alisema Mhe Membe.
Mhe. Membe aligusia pia mambo ya mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya nchi ya Tanzania na Malawi na amesema kuwa yeye pamoja Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mhe. Anna Tibaijuka na Mwanasheria walikwenda kuhudhuria mkuatno wa usuluhishi wa mgogoro huo na mpaka hivi sasa bado wapo katika hatua nzuri ya kusuluhisha ambapo ifikapo mwezi wa sita mwaka huu watakutana tena katika meza ya usuluhishi ili kutoa faida na hasara ya kuwa ndani ya mpaka na je ya mpaka katika ziwa hilo.
Waziri Membe alimalizia kwa kuwaasa watanzania kote nchini kupinga kutumiwa na watu katika biashara haramu ambako kunawapotezea maisha watanzania wengi na kuitia doa nchi yao kwa kumatwa kwao, hivyo ni vema wawe makini wanaposafiri nje ya nchi.
0 comments:
Post a Comment