Mkutano wa viongozi wa mataifa ya Kanda ya Maziwa Makuu mjini Luanda Angola
KWA mara ya kwanza marais wa nchi za Kanda ya Maziwa Makuu, ICGLR wamependekeza kuweko na vikwazo vya kisiasa na kiuchumi dhidi ya makundi ya wapiganaji yanayopatikana mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Kwenye mkutano wa siku moja mjini Luanda siku ya Jumatano viongozi hao Marais Edourdo dos Santos wa Angola, Dennis Sasou Nguesso wa Kongo Brazzaville,Yoweri Museveni wa Uganda, Joseph Kabila wa Kongo, na Paul Kagame wa Rwanda pamoja na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, aliyealikwa kuhudhuria, wameomba pia kurejeshwa haraka Kongo wapiganaji wa zamani wa kundi la M23 walioko Uganda na Rwanda.
Kwenye taarifa yao ya pamoja, marais sita wa nchi za Maziwa Makuu pamoja na Afrika ya kusini wamependekeza kuweko na mtizamo wa pamoja kwa ajili ya kupambana na makundi yote ya wapiganaji yalioko mashariki mwa DRC.
Ma rais hao wamepenekeza kuwawekea vikwazo vya kisiasa na kiuchumi viongozi wa makundi hayo ya wapiganaji.
Kukuza uhusiano na ushirikiano wa kikanda na kimataifa katika kufahamu mahala waliko viongozi wa makundi hayo ya wapiganaji ambayo bado ni tishio kwa usalama wa nchi za ICGLR.
Kuhusu hali ya usalama mashariki mwa DRC, rais Joseph Kabila aliwapa maaelezo marais wenzake kuhusu harakati za kijeshi zinanzoendeshwa na jeshi la Kongo dhidi ya waasi wa ADF kutoka Uganda. Na katika taarifa yao ya pamoja, marais wamepongeza mafanikio ya operesheni hizo na namna zinaendeshwa kwa ushirikiano na kikosi cha kikanda.
Mkutano huo wa marais ulizungumzia pia tatizo la kidiplomasia lililoko hivi sasa baina ya Rwanda na Afrika ya Kusini. Ilikua mara ya kwanza kwa marais Paul Kagame na Jacob Zuma kukutana tangu uhusiano baina ya nchi zao mbili kuzorota kufuatia hatua za kuwaondoa wanadiplomasia wao.
Rais Zuma aamewambia wandishi habari baada ya mazungumzo kwamba yeye na mwenzie wa Rwanda wamekubaliana kufanya mazungumzo ya moja kwa moja ilikumaliza ugomvi kati yao.
Umoja wa mataifa pia unaelezea kufurahishwa na operesheni za kijeshi dhidi ya waasi wa ADF,Kwenye mkutano na wandishi habari siku ya Jumatano mjini Kinshasa, msemaji wa kijeshi wa kikosi cha Umoja wa Mataifa,MONUSCO Lt kanali Felix Basse, amesema kwamba jeshi la Kongo limethibiti maeneo muhimu yaliokaliwa na waasi hao kwa zaidi ya miaka 6.
0 comments:
Post a Comment