Uwanja wa ndege wa Singapore Changi ulitajwa kuwa ni Uwanja wa ndege bora kwa mara ya pili katika orodha ya viwanja vya ndege bora duniani huko Barcelona, Spain.
Pia uwanja huu wa Changi ulishinda tuzo ya kuwa ni uwanja wenye huduma nzuri za kiburudani.
Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Korea ya kusini, sprawling Incheon, uliibuka kuwa ni namba mbili katika viwanja bora duniani kwa mara ya pili katika orodha hizo.
Pia ulishinda tuzo ya kuwa ni uwanja bora unaotoa huduma nzuri kwa wahamiaji na usafirishaji bora.
Uwanja wa ndege wa Munich ulishika nafasi ya tatu katika orodha ya mwaka huu na hiki si kitu cha kushangaza kwani uwanja huu una huduma nzuri ya vinywaji na bustani kwaajili ya kupumzikia wasafiri.
Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hong Kong umeshika nafasi ya nne katika orodha hiyo.
Pia uwanja huu umejishindia tuzo ya huduma bora za chakula na upokeaji wa mizigo
Uwanja wa ndege wa Amsterdam Schiphol umeshika nafasi ya tano, ambapo umerudi nyuma kwa nafasi mbili tofauti na mwaka jana.
Uwanja wa ndege wa Tokyo's Haneda umepanda kwa nafasi tatu na kushika nafasi ya sita mwaka huu.
Pia umekuwa wa kwanza kuwa ni uwanja msafi katika orodha hiyo.
Uwanja wa ndege wa mji mkuu wa Beijing umeshuka kwa nafasi mbili toka mwaka jana na kuwa namba saba mwaka huu katika orodha ya viwanja vya ndege bora duniani.
Uwanja wa ndege wa Vancouver umeshika nafasi ya nane.
Ukiwa ni kati ya viwanja vinavyojitengenezea umeme wake kwa njia ya mfumo wa nishati ya jua, Uwanja wa ndege wa Zurich umeshika nafasi ya tisa
Uwanja wa ndege wa London Heathrow umeendelea kushikia nafasi ya kumi na kujishindia tuzo ya kuwa kiwanja bora cha kufanya manunuzi.
0 comments:
Post a Comment