Sunday, March 2, 2014

NCHI ZA AFRIKA ZIMEJIFUNZA NINI JUU YA SHERIA  YA KUPINGANA NA USHOGA UGANDA?


BENKI ya Dunia na nchi za Ulaya zimepunguza utoaji wa misaada na mikopo nchini Uganda baada ya utata uliojitokeza hivi karibuni juu ya Muswada uliopitishwa unaopinga ushoga nchini humo.

Kitu pekee ambacho wengi wanajiliza kuhusu hili, ni je wananchi wa Uganda wataweza kukubali kubadilisha mawazo yao juu ya dhana ya ushoga nchini humo? 

Mnamo siku ya Jumatatu, Rais Yoweri Museveni alisaini moja kati ya sheria ngumu duniani inayopambana na ushoga.
Rais Yoweri Museveni akiweka saini kupitisha muswada huo unaopingana na vitendo vya mashoga
Jambo hilo limepelekea Benki ya Dunia na nchi kadhaa za Ulaya kusimamisha utoaji wa misaada na mikopo kwa nchi ya Uganda.

Sheria hiyo tata inapingana na vitendo hivyo vya jinsia moja kwa kutoa hukumu ya kifungo cha maisha kwa wale wote wataobainika wakishiriki katika matendo hayo (mashoga).
Sheria hiyo pia imewaomba wananchi kutoa taarifa juu ya wale wote wanaohusika na vitendo hivyo.
Kiongozi wa dini nchini humo akiongea na wananchi kuwahamasisha kuhusu jambo hilo
Si nchi ya Uganda pekee iliyopitisha sheria hiyo, bali nchi kama Nigeria na Urusi pia zimekuwa ni miongoni mwa nchi zilizopitisha sheria kama hiyo inayopingana na vitendo vya jinsia moja (mashoga)


Swali la kujiuliza ni kwanini Uganda ndio imekuwa ikinyooshewa vidole na chi za magharibi, na viongozi wa Afrika kupitia Umoja wa Afrika (AU) je wameupokeaje uamuzi huo wa serikali ya Uganda unaoongozwa na Yoweri Museveni.

Sheria hiyo imeamsha hisia nzito miongoni mwa wanauganda na baadhi ya watu walio nje ya Uganda, wengi wao wamejitokeza wakibeba mabango mbali mbali yanayowakilisha kile wanachoamini mioyoni mwao.
Kama inavoonekana katika habari picha:














0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI