Tuesday, March 4, 2014

12 YEAR'S A SLAVE PICHA BORA YA MWAKA TUZO ZA OSCAR

WACHAMBUZI wa filamu wameeleza kuwa ni muda sasa umepita tangu filamu kama hii iliyojaa kila sifa ya kushinda tuzo hiyo kupatikana, ambapo wameongeza kuwa inastahili tuzo hiyo kwa ubora wake wa picha.
Filamu ya '12 year's a slave' imeshinda tuzo ya filamu yenye picha bora kitu ambacho wengi walidhani filamu ya American Hustle na Gravity ndizo ambazo zingechukua tuzo hiyo lakini matarajio yao yalishangazwa kwa filamu hiyo kuibuka kinara wa tuzo hizo maarufu zaidi nchini marekani na duniani kwa ujumla.
Moja kati ya sehemu katika filamu hiyo inayoangazia maisha ya watumwa nchini 
Muongozaji wa filamu hiyo Steve McQueen aliamua kuielekeza filamu hiyo kwa wahanga wa utumwa miaka mingi iliyopita.

Filamu hii imejikita katika kuelezea maisha ya kitumwa waliyoishi mababu zetu miaka ya 1841...

HADITHI…
Filamu hii inamuhusu mtumwa huru mmoja ambaye alikuwa ni fundi seremala aliyekwenda kwa jina la  Solomoni Northup (Chiwetel Ejiofor) ambaye alikuwa akiishi na mkewe pamoja na watoto wao wawili katika eneo la Saratoga Springs huko jijini New York.

Wanaume wawili ambao ni Scoot McNairy na Taran Killam wakajitokeza na kumuahidi kumpa kazi jambo ambalo halikuwa kama ambavyo alitarajia kwani wanaume hao walimkamata na alipoamka na kupata fahamu zake akajikuta katika minyororo ambapo alikuwa tayari kwenda kuuzwa kama mtumwa. 

Kijana huyo akasafirishwa kwa njia ya meli mpaka New Orleans na alipofika huko akapewa jina la Platt na kununuliwa na mkulima mmoja ambaye alitokea kumkubali kijana huyo kwani alikuwa ni mfanyakazi hodari kitu ambacho kilimuudhi fundi selemara mmoja wa kizungu katika mashamba hayo ambaye akaanza kumfanyia vitendo vya kinyanyasaji Northup.

Kijana huyu anapitia mambo mengi ambayo ni ya kinyanyasaji na si ya kiungwana kwani aliuzwa mara kadhaa kwa wanunuzi wa watumwa na kukutana na mikasa kibao kwa muda wa miaka kumi na miwili na mwishoni akaokolewa na polishi mmoja ambaye alikuwa akiishi nae New York.
'Chiwetel Ejiofor' aliyeigiza kama 'Solomoni Northup'
Lupita Nyon'go aliyeigiza kama 'Patsey'
'Brad Pitt' kama 'Samuel Bass'
'Benedict Cumberbatch' kama 'William Ford'
'Michael Fassbender' kama 'Edwin Epps'
'Sarah Paulson' kama 'Marry Epps'
'Adepero Oduye' kama 'Eliza'

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI