Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiangalia ramani ya ujenzi wa miradi mitatu ya uwanja wa ndege wa Zanzibar, alipofanya ziara ya kutembelea miradi hiyo.
Mtathmini wa viwango vya ujenzi wa miradi hiyo Bw. Mohd Juma, akitoa maelezo mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais kuhusiana na ujenzi huo.
Meneja wa Mradi wa ujenzi wa njia za kupitia ndege wakati wa kuruka Frederick Nkya akionyesha ramani ya ujenzi huo.
Meneja wa mradi wa ujenzi wa jengo jipya la abiria bw. Ibrahim Zhang, akimueleza Maalim Seif hatua zinazoendelea za ujenzi huo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Miundo mbinu na mawasiliano, viongozi wa uwanja wa ndege wa Zanzibar pamoja na wakandarasi wa miradi ya ujenzi katika uwanja wa ndege wa Zanzibar.
(picha na Salmin Said, OMKR).
Habari na Hassan Hamad OMKR
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ameelezea kuridhishwa kwake na hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa miradi mitatu inayoendelea kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.
Miradi hiyo inahusisha ukarabati na ujenzi wa njia za kupitia ndege wakati wa kuruka pamoja na sehemu ya maegesho ya ndege, ujenzi wa uzio wa eneo la uwanja wa ndege, pamoja na ujenzi wa jingo jipya la abiria (Terminal 2).
Akizungumza katika ziara ya kutembelea miradi hiyo huko uwanja wa ndege wa Zanzibar, Maalim Seif amesema hatua iliyofikiwa inatia moyo, na kuwataka wakandarasi na wasimamizi wa miradi hiyo kuhakikisha kuwa inakamilika kwa wakati.
Amesema Serikali kwa upande wake itaweka mkakati wa makusudi ili iweze kumaliza kuwalipa fidia wananchi ambao bado hawajalipwa, na kuruhusu ujenzi wa uzio uweze kukamilika kwa akati.
0 comments:
Post a Comment