Kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Kamishna msaidizi wa polisi Ahmed Z. Msangi |
MTOTO AITWAYE IREENE MARCO MBEMBELA (07) MWANAFUNZI WA CHEKECHEA SHULE YA MSINGI MIGOMBANI NA MKAZI WA SOGEA ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU KATIKA KITUO CHA AFYA TUNDUMA.
MAREHEMU ALIPIGWA KWA KUTUMIA FIMBO SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE HADI KUPOTEZA FAHAMU NA BABA YAKE MZAZI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MARCO MBEMBELA (30) MKAZI WA SOGEA – TUNDUMA.
TUKIO HILO LILITOKEA TAREHE 19.03.2014 ALFAJIRI HUKO SOGEA KATA NA TARAFA YA TUNDUMA WILAYA YA MOMBA KWA TUHUMA KUWA ANATABIA YA KUZURURA OVYO KATIKA NYUMBA ZA WATU.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUTUMIA BUSARA KATIKA KUWAELEKEZA NA KUWAONYA WATOTO WAO BADALA YA KUWAPIGA KWANI NI HATARI KWA AFYA NA MAISHA YAO.
0 comments:
Post a Comment