Thursday, March 20, 2014

YUSUPH MLELA AIBUKIA KATIKA MCHEZO WA MASUMBWI KWA KUIPIGA TAFU KLABU YA MSISIRI

Msanii wa filamu nchini Yusuph Mlela (kushoto) akikabidhi sehemu ya vifaa vya mchezo wa ngumi kwa kocha wa klabu ya Msisiri, Daudi Muhunzi, ikiwa ni uboreshwaji wa klabu hiyo iliyopo CCM Msisiri Kinondoni Dar es salaam. Katikati ni mdau wa mchezo huo Ally Moja.
Na Mwandishi Wetu
MSANII wa filamu za bongo Yusuph Mlela, ameibukia katika mchezo wa masumbwi nchini na kuonyesha jitihada zake kwa kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya mchezo wa huo kwa Klabu ya ngumi Msisiri.

Baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na Gloves, Clip bandeji, Proctecta na GumShit.

Akizungumza baada ya kukabidhi msaada wa vifaa hivyo Mlela, alisema kuwa amevutiwa na vijana wa Klabu hiyo wanavyojitoa na kujishughulisha na mchezo huo na kuonyesha juhudi kwa kuupenda kwa kutenga muda wao mwingi kwa kufanya mazoezi.

''Vijana wenzangu waliniomba kuchangia Katika kata yangu hii ninayoishi nikaona ni jambo la busara na hasa ukizingatia ni moja ya kuwaokoa vijana wenzangu wengi wasio na ajira ambao wengi wameamua kujikita katika mchezo huu wa masumbwi''. alisema Mlela

Kocha wa mchezo wa ngumi katika Klabu ya Msisiri Daudi Muhunzi,  alimshukuru Mlela kwa kuwakumbuka vijana wenzie ambao walikuwa na uhaba wa vifaa vya mchezo huo.
Kwa hisani ya Sufiani mafoto blog

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI