Thursday, March 20, 2014

VIONGOZI MNAPOLETA MIZENGWE KATIKA KLABU, MNAWATESA WATU HAWA NYUMA YENU.

Unaanzaje kumwambia shabiki kama huyu, mwenye mapenzi makubwa na klabu yake ahamie timu nyingine. 
Lakini wapo watu wanaendesha klabu watakavyo, wanasahau kuwa kuna uwepo wa watu wenye hisia kali kama huyu jamaa. 
Unamtesa sana unapoleta longolongo nyingi kwenye mambo ya msingi yahusuyo timu. Usishangae kumuona kazimia au kazirai kwasababu ya mtu mmoja kuharibu mambo.
Hawachoki: Mashabiki wa Yanga walikuwa wenye furaha kubwa wakati klabu hiyo iko mbele kwa bao 1-0 jana uwanja wa Taifa, lakini mambo yalibadilika dakika ya 83 baada ya Kevin Friday kumtungua Juma Kaseja langoni
Hawa jamaa wanapokuja na njiwa au kuku uwanjani wanamaanisha nini?, au ndio mikwara kwa wapinzani?. Lakini njiwa hawa huwa hawaonekani pale timu inapofungwa.
Picha na Baraka Mpenja.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI