Monday, August 24, 2015

MSHINDI WA TMT 2015 #MPAKAKIELEWEKE

Mshindi wa TMT 2015 #mpakakieleweke, Denis Laswai akiwa ameinua mikono juu kuashiria ishara ya kumshukuru Mungu Mara baada ya Kutangazwa Mshindi wa TMT 2015 #mpakakieleweke msimu wa pili katika fainali iliyofanyika usiku wa kumkia leo katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar Es Salaam.
Mshindi wa shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2015 #mpakakieleweke Denis Laswai kutoka Kanda ya Kaskazini Arusha akiruka juu kwa furaha mara baada ya kutangazwa Mshindi wa Kitita cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania mara baada ya kuibuka kinara kwenye fainali hiyo ya TMT iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar Es Salaam.
Majaji wa Shindano la TMT wakifuatilia matukio yanayoendelea katika fainali ya shindano la TMT 2015 linaloendelea kufanyika katika ukumbi wa Makumbusho huku ikirushwa live kupitia Live na Kituo cha ITV
 Baadhi ya wahudhuriaji wakifuatilia matukio live
 Mshindi wa TMT #reachforthestars msimu wa Kwanza Mwanaafa Mwinzago akifurahia jambo mara baada ya Mshindi wa TMT msimu wa pili kutangazwa katika fainali ya TMT iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa
 Walimu wa washiriki wa TMT 2015 #mpakakieleweke Mwl Issa (Kushoto) akiwa na Mwalimu wenzake Dkt Mona Mwakalinga wakifuatilia shindano la TMT
 Mtangazaji wa Radio One/ITV Rehema Nyamaka (kulia) akiwa na shostito wake wakifuatilia shindano hilo lililokuwa likirushwa live na kituo cha Runinga cha ITV usiku wa Kumakia leo
 Meneja Mradi wa TMT Saul Mpock (Kushoto) akimpongeza Mshindi wa TMT 2015 #mpakakieleweke Denis Laswai (Katikati) huku akipongezwa pia na Bi Jennifer Kway, Mhasibu wa Kampuni ya Proin Promotions Ltd ambao ndio waandaaji wa shindano la TMT kwa Msimu wa Pili Sasa.
Baadhi ya wasanii mbalimbali wa tasnia ya filamu, wadau kutoka Basata na washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya ishirini bora wakifuatilia fainali hiyo.
 Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin, Mh Johnson Lukaza (Kulia) akimpongeza mshindi wa TMT 2015, Denis Laswai mara baada ya kutangazwa kuwa kinara wa TMT 2015 #mpakakieleweke
 Wadau wakiwa kwenye dhuria jekundu
Haji Mboto kazini
 Ruby akitoa burudani wakati wa fainali hiyo iliyofanyika usiku wa kuamkia leo na kupelekea Denis Laswai kutoka Mkoani Arusha Kuibuka Mshindi wa TMT 2015 #mapakkieleweke
 Watu mbalimbali wakifuatilia fainali ya TMT katika ukumbi wa makumbusho ya taifa usiku wa kumakia leo
Washiriki wa TMT 2015 #mpakakieleweke waliofanikiwa kuingia hatua ya kumi bora wakiwa mbele ya majaji na watazamaji wa fainali hiyo iliyokuwa ikirushwa live kupitia ITV.Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
Shindano la TMT hatimaye limefikia mwisho usiku wa kumkia leo katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa mara baada ya Kijana Denis Laswai kutoka Kanda ya Kaskazini Mkoani Arusha Kuibuka kidedea kwa kuwagaragaza Washiriki wenzie tisa waliofanikiwa kuingia hatua ya fainali na kuondoka na Kitita cha Shilingi Milioni Hamsini za Kitanzania huku washiriki tisa kuondoka na kifuta jasho mara baada ya shindano hilo kumalizika.
Shindano la TMT limechukua takribani miezi minne tangua kuanza kwa Mwaka 2015 huku likiwa limetembelea kanda sita za Tanzania na ha hatimaye kupata washindi wapatao 20 kutoka katika kanda hizo ambao waliingia katika mjengo wa TMT na kuanza kupatiwa mafunzo ya sanaa na walimu wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam
Mara baada ya washindi hao kupatikana na kuingia ndani ya mjengo wa tmt washiriki kumi waliweza kuaga mashindano hayo katika hatua ya mchujo na kubakiwa na washiriki wengine kumi ambao ndio waliofanikiwa kuingia hatua ya fainali.
Mara baada ya mshindi wa TMT 2015 #mpakakieleweke kupatika hapo usiku wa kumkia leo washiriki hao kumi watatengeneza filamu ya pamoja huku wakinufaika na filamu hiyo kuanzia utengenezaji wake hadi kuuzwa .
Mshindi wa TMT 2015 #mpakakielewe ni mshindi wa msimu wa pili wa shindano hili lililofanyika takribani kwa mwaka wa pili sasa huku Mshiriki wa kwanza kabisa akiwa ni Binti mdogo kutoka Kanda ya Kusini Mkoani Mtwara Mwanaafa Mwinzago ambae mara baada ya kushinda alipata nafasi ya kusomeshwa na kampuni ya Proin Promotions Ltd bila zawadi yake kuguswa. Washiriki kumi bora watakuwa chini ya mkataba wa kampuni ya Proin Promotions Ltd ambao ndio waratibu na waendeshaji wa shindano hili kubwa Afrika Mashariki na Kati huku shindano hili likiwa limepigwa tafu na Paisha, Pepsi, Camgas, Precision Air, Global Publishers, Data Vision International, I-View Studio, Van Maria Boutique, Hartman Barber Shop, na Hussein Pamba Kali

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI