Wednesday, November 16, 2016

RIPOTI YAONYESHA KUKOSEKANA KWA BUNGE ‘LIVE’ KUMEATHIRI WANANCHI

Na Emmy Mwaipopo
RIPOTI ya uchunguzi imebainisha kusitishwa kwa matangazo ya moja kwa moja kutoka Bungeni kumeathiri kwa kiasi kikubwa wananchi kwa kushindwa kufuatilia mijadala mbalimbali inayoendelea Bungeni pamoja na kutokujua nini wawakilishi wao wamewakilisha katika vikao vya bunge kwa faida ya wapiga kura.
Ripoti hiyo iliyopewa jina la nchi yetu, bunge letu uliofanywa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) ilizinduliwa jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Bahame Tom Nyanduga ambaye amesema ni uhuru kwa uhuru wa maoni ya watu.
“Taarifa ya kuzuia kwa matangazo ya moja kwa moja ya shughuli za bunge ni taarifa iliyosheheni uchunguzi ulioonyesha faida na hasara wa uamuzi huo,ukiondoa suala la gharama ambalo pia limechambuliwa na kuonekana kwamba matangazo yangeweza yakaendelea kupitia hata vyanzo visivyo vya kiserikali kimsingi taarifa inaonyesha uzoefu wa nchi mbalimbali unaonyesha kuwa matangazo hayo ni kitu bora kwa jamii,
Taarifa hii inaweza kusaidia viongozi wanaohusika na maamuzi hayo kuona ni jinsi gani uhuru wa maoni ni muhimu kuliko gharama
Utafiti huo ulihusisha wananchi, wamiliki wa vyombo vya habari na baadhi ya wabunge tangu kusitishwa kwa matangazo ya moja kwa moja ambapo moja kati ya watafiti ambaye ni meneja mipango kutoka baraza la habari Tanzania Bi Pili Mtambalike ameeleza matokeo ya ripoti hiyo.
“Kutokana na kuongea na wananchi tuliona kuwa kabisakabisa walionyesha kuwa kusitishwa kwa matangazo ya moja kwa moja kumeathiri sana uelewa wao wa mambo ambayo yanaendelea bungeni hivi sasa wako kwenye kiza hawajui sana kile kinachoendelea kwasababu tu ya kusitishwa kwa matangazo ya moja kwa moja,” alisema Bi Pili.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI