Sunday, November 6, 2016

REKODI YA SIMBA IMEVUNJWA NA AFRICAN LYON LEO NOVEMBER 6 2016

LIGI Kuu soka Tanzania bara msimu wa 2016/2017 umeendelea tena leo November 6 2016 kwa michezo sita kupigwa katika viwanja mbalimbali, kwa upande wa Simba wao walikuwa uwanja wa Uhuru kucheza dhidi ya wenyeji wao African Lyon.
Simba wakiwa wameingia katika uwanja wa Uhuru wakiwa na kumbukumbu ya kutopoteza mchezo msimu huu katika mechi zake 13, leo kwa mara ya kwanza wamekubali kuziachia point tatu dhidi ya African Lyon, wengi walikuwa wanajua Simba watatoka na ushindi kutokana na African Lyon kutokuwa katika kiwango kizuri zaidi ya Simba.
Mchezo umechezwa na Simba kiasi kikubwa aliutawala mchezo na kuwashambulia African Lyon ambao walionekana kucheza mchezo wa kujihami zaidi, lakini dakika nne za nyongeza kabla ya mchezo kumalizika Abdullah Msuhi akapachika goli la ushindi kwa African Lyon ambapo mchezo ukafanya umalizike kwa Lyon kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI