Makaa nchini Somalia ambayo wanajeshi wa Kenya wanatuhumiwa kutoza kodi
Kenya imetupilia mbali tuhuma nyengine kwamba wanajeshi wake wananufaika kutokana na mkaa unaosafirishwa kutoka Somalia biashara ambayo imeendelea hata baada ya Umoja wa Mataifa kutaka ipigwe marufuku.
Msemaji wa rais (Manoah Esipisu) alieleza kuwa, inaonesha ripoti ya Umoja wa Mataifa inagusia tuhuma za zamani za mashirika yasiyokuwa ya serikali, na nia ya madai hayo ni kuwavunja moyo wanajeshi wa Kenya.
Ripoti ya Umoja wa Mataifa ilikiisia kuwa jeshi la Kenya lilikuwa linapata takriban dola milioni 12 kila mwaka, kwa kutoza ushuru mkaa unaosafirishwa kupelekwa nchi za nje.
#BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment