Saturday, November 12, 2016

OMMY DIMPOZ - 'MASHABIKI HAWAJUI, KUKAA KIMYA KWENYE MUZIKI SIO KUPOTEA KWENYE MUZIKI'

MUIMBAJI Ommy Dimpoz amesema ukimya wake kwenye muziki sio kwamba alipotea bali alikuwa anafanya mambo mengine nje ya muziki.
Ommy Dimpoz amesema watanzania wamekuwa na mtazamo tofauti sana hasa pale msanii anapokuwa kimya kwenye kazi zake, na kukimbilia kumlaumu.
“Mimi nilikuwa kimya nilikuwa nafanya mambo yangu mengine, lakini sio kama kukaa kwangu kimya nilikuwa nimepotea kwenye muziki,” Ommy aliiambia FNL ya EATV. “Unajua watanzania wamekuwa na tafsiri tofauti, kuna watu wanatake break akina Justin Timberlake wanakaa miaka 7, na mimi nilikuwa zangu vacation, ma Ibiza huko, sasa nimerudi nataka kufanya kazi”,
Muimbaji huyo amerudi na wimbo Kajiandae akiwa ameshirikiana na AliKiba.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI