NGULI wa filamu, Ahmed Olotu maarufu kama ‘Mzee Chilo’ amesema licha ya tasnia ya filamu kukumbwa na changamoto nyingi lakini wasanii wa filamu wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii na kuacha kulalamika.
Mzee Chilo aliiambia Bongo5 kuwa wasanii hawatakiwi kukata tamaa kwa kuwa tayari wameitoa mbali tasnia ya filamu.
“Mimi napenda kuwaambia wasanii wenzangu tufanye kazi kwa bidii,” alisema Chilo. Haya mambo ya kulalamika tupunguze na hiyo nguvu tuipeleke katika kufanya kazi kwa bidii hata wao atakapokuja watakuta tumeshafika mbali kuliko kuendelea kulalamika na wengine kukata tamaa,”
Aliongeza, “Bado tasnia ya filamu tunaijenga, ndio maana hata tulikuwa tunaitaka serikali iitambue sanaa kama kazi ramsi. Kwa hiyo mimi bado naona mambo mazuri yatakuja huko mbele.,”
Mwigizaji huyo ambaye ana umri wa miaka 65, amewahi kutamba kwenye filamu nyingi bongo pia alijipatia umaarufu mkubwa kupitia Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu iliyokuwa ikirushwa na kituo cha TBC 1, enzi hizo TVT.
0 comments:
Post a Comment