Saturday, January 24, 2015

TAHADHARI *PICHA* ZINATISHA: RISASI ZARINDIMA DARAJANI ZANZIBAR

POLISI wenye silaha, wakiwa tayari kukabiliana na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi mapema leo Ijumaa, Januari 23, 2015, kwenye eneo maarufu la kibiashara, Darajani kisiwani Unguja Zanzibar. Mashuhuda wanasema,
watu wanne wenye silaha wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakijaribu kufanya uporaji, kwenye eneo hilo, walikabiliana vilivyo na polisi, ambapo walijibizana risasi na kuzua mtafaruku mkubwa kwenye eneo hilo.
Ripoti zisizokuwa rasmi zinasema mtu mmoja alipigwa risasi na anasadikiwa kuuawa katika mapambano hayo yaliyodumu kwa dakika kadhaa. Habari pia zinasema, watuhumiwa hao, waliteka magari na kujaribu kukimbia, ambapo katika tukio hilo, waligonga raia wema watembea kwa miguu. Polisi wamefanikiwa kuyatia mbaroni majambazi hayo na magari waliyotumia kufanya uhalifu huo.
Hivi ndivyo ilivyokuwa mapema leo Ijumaa januari 23, 2015
Mmoja wa watuhumiwa wa ujambazi katika maeneo ya darajani akiwa chini ya ulinzi wa Polisi akiwa katika gari waliokuwa kulitumia kwa ujambazi huo.aina ya Rav4. na nyengine aina ya Noah.
Wananchi wakiwa na hasira wakiwa katika mtaa wa darajani wa wakishuhudia jeshi la Polisi Zanzibar kuzima jaribio la ujambazi katika maeneo ya darajani makonte, na kuwadhibiti majambazi watatu wakiwa katika harakati za kuvamia katika maeneo hayo kwa kutaka kupora, majambazi wawili wamekamatwa na mmoja kukimbia.
Wananchi wakishuhudia tukio la kufanyika kwa ujambazi katika maduka ya darajani.
Mtuhumiwa wa ujambazi akiwa ndani ya gari ya Polisi baada ya kupata kipigo kutoka kwa Wananchi wenye hasira wakati wakiwa katika harakati za kutaka kukimbia jirani na skuli ya Darajani baada ya kutelekeza gari waliokuwa wakiitumia aina ya Noah.
Gari aina ya Noah linalosadikiwa lilitumika katika tukio la ujambazi katika maeneo ya darajani likiwa limetelekezwa baada ya watuhumiwa hao wakiwa katika harakati za kuwakimbia Askari katika eneo la mbele ya skuli ya Darajani.
#ZanziNews

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI