Friday, November 11, 2016

FID Q ASEMA SOKO LA ALBUM BADO LIPO ILA MASHABIKI HAWAJUI WATAZIPATA WAPI!

RAPPER Fareed Kubanda aka Fid Q amesema soko la album hapa Tanzania bado lipo hai, ila mashabiki hawajui watazipata wapi.
Alikuwa akiongea kwenye kipindi cha Ladha 3600 cha EFM Alhamis hii.
Fid amesema mashabiki hujikuta wakitafuta kazi za wasanii zilizokusanywa kienyeji kwasababu hakuna sehemu wanaweza kupata halali.
“Ni kwasababu wanakosa access lakini hawa watu wanatufeel, wanajua kabisa kwamba mimi nisiponunua album ya Fid Q atazeeka katika nyumba ya kupanga ntakuwa sina sababu ya kumcheka kwasababu mimi nimehusika katika umaskini wake,” alisema Fid.
Fid alisema ukweli huo ulimfanya ashindwe kufanya chochote baada ya kukutana na mtu akiuza CD yenye mkusanyiko wa video ukiwemo wimbo wake Roho aliofanya na Christian Bella.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI