Friday, November 28, 2014

MR. & MRS. NZOWAH WASHEREHEKEA MIAKA MITANO YA NDOA YAO *PICHAZ*

ILIKUWA ni tarehe 26/11/2009 Siku ambayo Bw. Meshack Nzowah alifunga ndoa na Bi. Asha Farahani ambapo kwa pamoja walikubaliana kuishi kama mke na mume, siku iliyokuwa ni furaha sana kwa wawili hao kwani iliambatana na hafla fupi iliyofanyika landmark Hotel.
Maneno mazuri toka kwa wawili hao yalikuwa ni wote kwa pamoja kuoneshana mapenzi makubwa na kifo tu ndio kiwatenganishe, kitu ambacho mpaka sasa kinaonekana.
Hivi karibuni wawili hawa wametimiza miaka mitano ya ndoa yao ambapo Mungu amewajaalia mtoto mmoja aitwaye Nadir Nzowah.
Bw. Meshack Nzowa akiwa ni Mtangazaji wa TV 1 Tanzania na Bi. Asha akiwa ni mfanyakazi wa Lake Oil, wawili hawa wanakuwa mfano kwa vijana wengi ambao wanatamani kufikia mahali wanandoa hawa walipo.
Nadir Nzowah.
Kila La Kheri Familia ya Nzowah katika safari ya maisha.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI