Thursday, November 10, 2016

DULLY SYKES - 'NABADILIKA KADRI MUZIKI UNAVYOBADILIKA'

Na CHRIS BEE (EBONY FM)
THE Legend na Hitmaker wa INDE, Dully Skyes amedai kuwa ni msanii mkongwe anayejivua gamba kila muziki wa Bongo unavyobadilika.
Amesema hiyo ndio sababu inayomfanya aendelea kufanya vizuri hadi sasa.
“Kila kitu kuanzia uvaaji, kunyoa vile nilivyo naonekana kama wa leo, hata muziki wangu naimba wa kileo, siimbi tena muziki wa kizamani, kwa sababu zamani tulikuwa tunafanya muziki mzuri, sauti nzuri, beat nzuri, na vile unavyofanya show vizuri lakini siku hizi Kiki imekuwa ndio kila kitu ila mimi siwezi kwenda na Kiki nitafanya muziki tu ili mradi nijulikane,” amesema.
“Mimi kama mimi kwanza umri wangu umekwenda kwahiyo nikitaka kufanya kitu kama Kiki vitaniangusha,” Dully amepigia Mstari kupitia kipindi cha The Splash kinachoruka kupitia Ebony FM.
Katika hatua nyingine muimbaji huyo ameelezea kusikitishwa na wasanii kuendelea kutumia dawa za kulevya licha ya kuwa wanajua kuwa yanaathiri maendeleo ya kimuziki, afya na akili.
“Kiukweli wasanii wengi wa zamani na wapo wasanii tunao madawa ya kulevya yamewaharibu kabisa katika vichwa vyao, wasanii wa zamani watu wazima lakini bado wanaendelea na madawa wanaongea ovyo ovyo wanaropoka kwaajili ya dawa wanakuwa wanaharibika wanashindwa kufanya vizuri,” anasema.
Dully Sykes ameongeza kuwa yeye hawezi kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya kwakuwa ana familia.

“Mimi napambana kwa sababu nina familia, na watoto zangu, wadogo zangu na nina mama yangu, wote wananiangalia sasa nikitaka kuingia sitokuwa mtu tena nitakuwa balaa, familia yangu itaishi vipi sasa mtu kama hutakuwa na majukumu basi unaweza kufanya vitu vya kipumbavu.”

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI