Thursday, November 10, 2016

RAIS MAGUFULI AONGOZA KUAGWA KWA MWILI WA MAREHEMU JOSEPH MUNGAI *PICHAZ*

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli amewaongoza waombolezaji kuaga mwili wa marehemu Joseph Mungai kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, Alhamis hii.
Msiba huo umehudhuriwa na viongozi wengine wa serikali akiwemo Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, Jaji Joseph Warioba, Dk Augustine Mahiga, William Lukuvi, Fredrick Sumaye Steven Wasira, Mama Salma Kikwete, Makamu wa Rais Mstaafu, Mohamed Gharib Bilal na wengine.
Mungai aliwahi kuwa Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mkoani Iringa lakini pia aliwahi kuwa Waziri katika wizara mbalimbali kuanzia serikali ya awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere hadi ile ya awamu ya nne ya Jakaya Kikwete. Atazikwa Ijumaa hii nyumbani kwao Mufindi.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI