MSANII wa muziki na mtayarishaji wa ‘High Table Sound’ Barnaba Classic amesema mwezi January 2017 atatangaza mabadiliko makubwa ya label yake.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo Lover Boy, amesema kwa sasa wanajitahidi kuupush wimbo mpya wa msanii wa label yake aitwae Mulla.
“Kwa sasa mimi sina mpya lakini label yangu ‘HighTable Sound’ imeachia kazi mpya ya msanii Mulla, wimbo unaitwa Waniwasha akiwa amenishirikisha mimi,” alisema Barnaba.
“Lakini mambo makubwa zaidi yanakuja mwezi January, hapo nitatangaza mabadiliko makubwa ya label yangu pamoja na kuongeza wasanii wapya na mambo mengine. Kwa hiyo mashabiki wa Barnaba wasubirie mambo mazuri kutoka kwangu pamoja na kwa wasanii wangu,”
Muimbaji huyo alikuwa mmoja kati ya wasanii ambao walifanya vizuri katika tamasha la fiesta lililofanyika weekend iliyopita.
0 comments:
Post a Comment