Sunday, September 13, 2015

KITUO CHA SOUND CITY NIGERIA KIMESITISHA KUCHEZA KAZI ZA P SQUARE, BEEF!!!? SABABU IKO HAPA!

KITUO kikubwa cha television kinachocheza video za muziki muda wote nchini Nigeria kimewafungia wasanii P Square na video zao hazitachezwa kwenye kituo hicho.
Jambo hili limefanyika toka mwaka 2014 na kwa mujibu wa Sound City ''P Square waliombwa wafanye show na kituo hicho ila walishindwa kukubaliana malipo'' Sound City imesema meneja wa P Square alijibu vibaya sana alivyombwa kupunguza bei, jibu lake lilikuwa Kwani Sound City imesaida nini P Square, tuambie kitu kimoja tu”.
Sound City imecheza na kutoa ushirikiano kwa P Square kwa miaka kumi na jibu hilo lilichukuliwa kama dharau kwao na ndio wakasimamisha kucheza video za P Square.

P Square wamewaambia mashabiki wao waache kuifuatilia channel hio.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI