Tuesday, August 18, 2015

ZARI THE BOSSLADY AWAJIBU IVAN NA KING LAWRENC, ‘VISASI HUFANYWA NA VILAZA’

HATIMAYE Zari The Bosslady ameamua kumjibu ex wake Ivan na swahiba wake King Lawrenc ambao wamekuwa wakimtupia madongo kuwa mtoto wake Tiffah si wa Diamond, ni wao.

King Lawrence alienda mbali zaidi kwa kutumia kampuni ya wanasheria kumtaka achukue vipimo vya DNA vya kichanga hicho chenye zaidi ya followers 80k kwenye Instagram.

Zari ametumia Instagram kuwajibu kwa kudai kuwa wanachofanya wawili hao ni visasi ambavyo anaamini hufanywa na vilaza!

Visasi hufanywa na vilaza,” ameandika Zari kwenye Instagram.

BO$$LADY anafahamu kuwa huzuni aliyonayo mtu mwenye chuki wakati akiangalia furaha na mafanikio yake ni adhabu tosha. Inabidi niyageuzie mgongo mambo yate ya kijinga yanayoendelea. Naendelea kuwaua kwasababu watu hutaka kuzima taa inayowaka zaidi kwao,” ameongeza.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI