Kocha
wa Crystal Palace Alan Pardew anaamini kwamba Arsenal wamefanya kosa
kubwa kutomsajili kiungo wa klabu hiyo Yohan Cabaye wakati akihama
kutoka klabu ya PSG msimu huu wa majira ya joto.
Arsenal
walijaribu kumsajili Cabaye mwezi January mwaka 2014, wakati akiwa
Newcastle kabla ya kutua PSG ambako kukosa nafasi ya kucheza katika
kikosi cha kwanza cha Laurent Blanc, kumemfanya Mfaransa huyo kuamua
kurudi kukipiga EPL kwa mara nyingine tena.
Lakini
Pardew, kwa upande wake bado anaamini kuwa Cabaye ana uwezo wa kutosha
kuichezea Arsenal, na hivyo anajihisi ni mwenye furaha kuweza kumpata
kiungo huyo maridadi ambaye hapo awali alifanya naye kazi akiwa
Newcastle.
"Nadhani
angefanya makubwa sana pale Arsenal, lakini ni lazima tuwe tu wakweli,
huyu kijana ana uwezo mkubwa sana katika eneo la kiungo, sidhani kama
angeenda Arsenal eti angekosa nafasi katika kikosi cha kwanza, maana kwa
kipindi ambacho angekaa klabuni hapo basi angezoeana na wenzake na
kufanya mambo makubwa tu", Pardew aliwaambia waandishi.
"Ni
mchezaji wa ajabu sana, tunajisikia ni wenye furaha kubwa kumpata na
naweza kusema kuwa ni mchezaji wa kiwango cha Arsenal kabisa huyu. Hivyo
sidhani kama Arsene Wenger ama mtu mwingine yeyote pale Arsenal ambaye
anaweza kupingana na hilo.
"Tuna mchezaji ambaye angeweza kucheza pale kwao, hivyo hilo ni jambo jema kwetu".
0 comments:
Post a Comment