Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limetoa kauli kuwa adhabu ya kufungiwa kutojihusishwa na sanaa kwa mwaka mmoja ndani na nje ya nchi msanii Shilole ipo palepale, kauli ya hiyo imekuja baada ya msanii huyo kusema kuwa atakwenda kufanya shoo nchini Marekani pamoja na msanii mwenzake Ommy Dimpozi licha ya kufungiwa kwa mwaka mmoja.
Akiongea na East Afrika Radio Shilole alisema amejiandaa vizuri sana katika shoo ambayo anapaswa kuifanya nchini Marekani siku za karibuni, na alipoulizwa atawezaje kufanya shoo hiyo wakati akiwa amefungiwa na BASATA, Shilole alionekana kupaniki na kubadilika na kumwambia mtangazaji kuwa yeye hataki kuzungumzia suala la adhabu iliyotolewa na BASATA na kusema suala hilo anapaswa kuulizwa mwanasheria wake Albert Msando.
Hata hivyo kwa upande wa BASATA, Afisa Habari wa baraza hilo, Bw. Basyeibya amesema adhabu ya msanii huyo ipo palepale na wao wanaamini kwamba msanii Shilole anaitekeleza adhabu hiyo na
iwapo atakiuka adhabu hiyo watachukua hatua nyingine zaidi mbele.
"Adhabu ya Shilole iko wazi kwa maana ya kuzuiwa kufanya onyesho ndani na nje ya nchi utakumbuka kuwa kosa ambalo lilimfanya kufungiwa alilifanya nchini Ubelgiji kwa hiyo adhabu yake ipo pale pale haijatenguliwa hivyo hatakiwi kufanya onyesho lolote ndani au nje ya nchi, “alisema Bw. Basyeibya na kuongeza kuwa, “Kama anaweza kukiuka adhabu hiyo sisi Basata iwapo atakiuka adhabu hiyo tutachukua hatua zaidi dhidi yake".
Eatv.tv
0 comments:
Post a Comment