KAZI nzuri iliyofanywa na Winga machachari wa Yanga Simon Msuva, imeiwezesha timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya timu ya Taifa Jang'ombe katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi uliomalizika hivi punde kwenye uwanja wa Aman Mjini Zanzibar.
Mabao matatu kati ya manne yalifungwa na Simon Msuva katika dakika ya 13 bao la kwanza, bao la pili dakika ya 49 na la tatu katika dakika ya 63, huku bao la nne likifungwa na Kpah Sherman katika dakika ya 90+.
Aidha katika mchezo huo Msuva alizawadiwa mpira na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Zanzibar (ZASWA) na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo.
0 comments:
Post a Comment