Sunday, December 14, 2014

MBUNGE MACHACHARI KUTOKA LUDEWA DEO FILIKUNJOMBE (CCM) AWANUSURU KIAFYA WAKAZI WA DODOMA, AWAPA MSAADA WA VIFAA VYA MAJI VYENYE THAMANI YA ZAIDI YA TSH MILIONI 14.5 *PICHAZ*

Mbunge wa  jimbo la  Ludewa Deo Filikunjombe akinywa maji kwa majani ya miti baada ya kuzindua mradi wa maji na kukabidhi vifaa vya kuvuta maji  vyenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 14.5 kwa wakazi wa kitongoji cha Dodoma kijiji  cha Amani Ludewa
Mbunge wa Ludewa  Deo Filikunjombe akisoma maandishi mara baada ya kuzindua mradi wa maji kitongoji cha Dodoma kijiji cha Amani.
Mbunge   Filikunjombea  akifurahia  utamu wa maji 
Mbunge  Filikunjombe kushoto  akifurahia utamu wa maji 
Mbunge wa  Filikunjombe na viongozi wa  kitongoji cha Dodoma kijiji cha Amani  wakipanda mlima  mkali  pindi  walipotoka  kutazama  chanzo cha maji 
Upandaji wa mlima  kutoka kwenye chanzo cha maji ulivyomtesa mbunge Filikunjombe 
Mbunge Filikunjombe akijiandaa  kuruka korongo 
Wananchi  wa kitongoji cha Dodoma  wakifurahia maji 
Wanawake wa kitongoji cha Dodoma kijiji  cha Amani wakiwa  wamemkumbatia  mbunge  wao Filikunjombe kwa furaha  baada ya kutimiza ahadi ya maji 
Mbunge  Filikunjombe mwenye  kijani kulia  akikabidhi  baadhi ya  vifaa vya maji kwa wananchi wa kitongoji cha Dodoma Ludewa 
Wananchi akifurahia vifaa  hivyo 
Baadhi ya  vifaa  hivyo 
Mbunge Filikunjombe  akiwahutubia  wananchi hao kwa   furaha 
.Mbunge  wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe  akiwahutubia  wananchi wa kitongoji cha Dodoma kijiji cha Amani wilayani Ludewa baada ya  kukabidhi vifaa vya maji  vyenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 14.5 jana  huku mmoja kati ya  wanawake  wa  kijiji  hicho akiwa amelala miguuni mwake kama sehemu ya  kushukuru kwa msaada  huo 
Wananchi  wakifurahia  wakati  mbunge  Filikunjombe akiwahutubia 
Furaha  ya kupata  maji 
Mkazi  wa  kitongoji  cha Dodoma Bi Belinada Mwenda akimshukuru  mbunge wa  Ludewa  Deo Filikunjombe kwa msaada  wa maji 
Wananchi  wa  kitongoji cha  Dodoma kijiji  cha Amani  Ludewa  wakimzawadia zawadi ya mkungu wa ndizi mbunge  wao Deo Filikunjombe baada ya  kuwasaidia msaada wa vifaa vya maji  vyenye thamani ya Tsh milioni 14.5
Na MatukiodaimaBlog
WANANCHI  wa  kitongoji  cha Dodoma kijiji  cha Amani  wilaya ya Ludewa  mkoani Njombe kuondokana na kero ya maji  safi na salama baada ya mbunge wa  jimbo la  Ludewa Deo Filikunjombe kuwatimizia ahadi yake ya vifaa  vyenye thamani  ya  zaidi ya Tsh milioni 14. 5 kwa ajili ya kuvuta na  kusambaza maji safi na salama  ya  bomba katika  kitongoji  hicho .

Akishukuru  kwa niaba ya  wananchi  wengine  wakati wa hafla ya  kukabidhiwa  vifaa  hivyo jana Bi Belinada Mwenda  alisema  kuwa awali wananchi wapatoa zaidi ya 600 wa  kitongoji   hicho ambacho  kimeanzishwa na jamii ya  wachimbaji wa madini ya dhahabu  ,walikuwa  wakitumia maji machafu  yanayotumika  kuoshea madini na kunyweshea mifuko .

Hivyo  alisema  kuwa  msaada  huo  wa maji  safi na  salama utasaidia  kuwaepusha na magonjwa na milipuko kama kuhara  na mengine ambayo  walikuwa wakiyapata kutokana na matumizi ya maji yasiyo salama kwa afya  ya  binadamu kwa  kipindi  chote cha zaidi ya miaka 10  sasa  toka  kitongoji  hicho  kilipoanzishwa mwaka 1992.

" Hakika  tunakushukuru  sana  mbunge wetu  kwa kutusaidia msaada  wa vifaa hivi kwa ajili ya maji .....toka  mwaka 1992  hadi  leo tumekuwa  tukiteseka kwa  magonjwa mbali mbali na hata  baadhi  yetu  kupoteza maisha  kutokana na matumizi ya maji machafu ambayo tulikuwa tukitumia maji ambacho  kimsingi yalikuwa ni mabaki ya maji yanayobaki katika kunyweshea mifugo na kuoshea madini"

Bi Mwenda  alisema  wananchi hao  mbali ya kero  kubwa ya maji ambayo  walikuwa  wakiipata ila  bado walionyesha uaminifu kwa mbunge  wao  kwa kuendelea kubaki ndani ya CCM hadi sasa  wanapotimiziwa ahadi  yao  hiyo kwa kitongoji   hicho  kuwa ni moja kati ya vitongoji  vyenye msimamo na mbunge  wao kwa  kutoviunga mkono  vyama  vya  upinzani .

" Kwa shida tuliyokuwa  tukiipata kama  maeneo mengine leo wote  tungekuwa tumejiunga na  upinzani ila tuliamini chama  pekee ambacho kinaweza  kutusaidia na CCM na ndio  sababu hatukuona sababu ya  kujiunga na vyama  vya upinzani .....mheshimiwa mbunge  wetu tunakuhakikishia kuwa kitongoji  hiki hakuna hata  mwananchi  mmoja ambae ni upinzani na  wala hatuna mpango  wa  kuhangaika na vyama sisi  tutabanana  hapa hapa CCM"

Akizungumza na  wananchi  hao mbunge Bw Filikunjombe pamoja na kuwapongeza  kwa kutojiunga na vyama  vya upinzani  bado  alisema  kuwa ameguswa kutimiza ahadi yake kwa  wakati  kutokana na mateso makubwa ambayo wananchi hao  walikuwa  wakiyapata kwa  kukosa  huduma ya maji  safi na  salama .

Kwani  alisema  kuwa  lengo la  serikali ya CCM iliyopo madakarani  chini ya Rais Dr Jakaya  Kikwete ni kuona watanzania  wanaendelea  kuboreshewa mazingira ya maisha  yao na hata  kupunguza baadhi ya kero  zinazoweza  kupunguzw kwa  wakati  uliopo  na ndio  sababu ya yeye kama mbunge pia  kuendelea kukimbiza kasi ya maendeleo ya jimbo  hilo la Ludewa na kamwe hatakubali  kuona  wananchi  wake  wakiendelea kuteseka.

"Ndungu  zangu  wananchi  wa  kitongoji   hiki  cha Dodoma katika  kijiji hiki cha Amani nimewapenda  sana na ninyi  wenyewe  mnatambua kuwa mimi mbunge  wenu nawapenda ..... hivyo msaada  huo  leo ni utekelezaji wa ahadi yangu  niliyoitoka miezi  michache  iliyopita  nikiwa kama  mbunge  wenu japo siku  nilipotoa ahadi  hii  baadhi yenu hamkuweza  kuamini kama leo  ingetekelezwa ...nawaombeni  sasa tunzeni vema  vifaa hivi na  kutunza  zaidi mazingira  ili kufanya  chanzo cha maji  kuendelea kuwa hai  zaidi "

Mbunge Filikunjombe  alivitaja  vifaa ambavyo amevitoa ni pamoja na bomba za maji ambazo  zitasambazwa katika  kitongoji  chote kutoka kwenye chanzo  cha maji  zaidi ya kilometa 20 hadi  kwenye  kitongoji  hicho .

Kuhusu wafugaji  wanaochungia mifugo katika chanzo  cha maji mbunge  huyo aliwataka  wananchi na  viongozi hao  kuweka  sheria ya  kulinda chanzo   hicho  cha maji vinginevyo hakutakuwa na maana ya  kuwa na bomba  za maji  safi ambazo zitaingiliwa na mifugo.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI